Serikali imesema imepokea
kwa masikitiko taarifa za kuzama kwa Kivuko cha mto kilombero na kewamba
kamati za ulinzi na usalama zipo katika eneo hilo kuhakikisha hali
inarejea salama katika eneo hilo.
Hayo yamesemwa Bungeni na
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu)
Jenista Mhagama baada ya kutakiwa afanye hivyo na naibu spika wa Bunge
Tulia Mwansasu kuhusiana na suala hilo.
Mheshimiwa Naibu spika
serikali imepata taarifa hizo kwamba kivuko hicho kilikuwa kimebeba watu
31 na magari na mizigo mbalimbali na kilizama jana usiku ambapo watu 30
wameokolewa huku jitihada mbalimbali zikiendelea kuleta usalama katika
eneo hilo.
Aidha Waziri Mhagama
amewataka wananchi kuwa makini kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa nchi
itapata mvua nyingi sana pamoja na upepo mkali hivyo ni vyema wasafiri
wakawa makini katika maeneo mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment