Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani.
Serikali imesema kukosekana kwa fedha za kutosha kumechangia baadhi ya miradi ya maendeleo kusimama ikiwano ya barabara.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Edwin Ngonyani, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilombero
(Chadema), Peter Lijualikali, aliyetaka kujua ni lini serikali itapeleka
fedha kwa mkandarasi ili aweze kumaliza ujenzi wa daraja la Kilombero.
Ngonyani alisema fedha za ujenzi wa daraja hilo zinatolewa na
serikali kwa asilimia 100 lakini haiwezi kukamilisha miradi yote kwa
wakati mmoja kutokana na uwezo wa mdogo wa ukusanyaji wa mapato ya
ndani.
Alisema ujenzi wa daraja hilo unatarajia kukamilika Desemba mwakahuu.
Akijibu swali la msingi lililohoji ni lini seriklai itaanza
kumaliza ujenzi wa barabara ya Kidatu, Ifakara na Mlimba kwa kiwango cha
lami.
Alisema barabara ya Kidatu hadi Ifakara mradi huo umeanza
kutekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha na katika awamu
ya kwanza na ya pili jumla ya kilomita 16.17 zilijengwa na kukamilika
kwa kiwango cha lami.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment