Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wabunge wa Upinzani
wameendelea na mgomo wao wa kutoka nje ya ukumbi wa bunge baada ya kikao
cha bunge kumaliza muda wa maswali na majibu kwa serikali.
Hali hiyo imetokea baada ya
Naibu Spika Tulia Mwansasu amemtaka katibu wa bunge kuarifu bunge
ratiba inayoendelea, ambapo katibu wa bunge alibainisha kwamba kazi ya
ratiba ya leo inaonyesha kwamba ni kuchangia hotuba ya Rais aliyoitoa
wakati wa ufunguzi wa bunge.
Baada ya hapo wabunge wa
upinzani waliomba miongozo kutoka kwa Naibu spika ambapo Naibu spika
amemruhusu Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko ambapo Mbunge huyo
ameuliza swali kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa elimu bure kwa
wanafunzi kutozwa michango katika jimbo lake.
Naibu wa spika akitoa
majibu ya muongozo huo ambapo amesema kwamba serikali inatanbua matatizo
yanayojitokeza na inayafanyia kazi
Jambo hilo limewakasirisha
wabunge wa upinzani na kuzidi kuomba miongozo ambapo Naibu Spika
amewakataza na kuruhusu ratiba iliyo mbele ya bunge kuendelea,hali
ambayo imewafanya wabunge wa upinzani kutoka nje.
Hata hivyo wabunge wa
upinzani baada ya kutoka nje hapo jana walishinikiza kwamba hawawezi
kukubali serikali kuendesha mikutano ya Bunge bila kuonyesha live kwa
kisingizio cha fedha kukosekana.
0 comments:
Post a Comment