Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha.
Serikali inapanga kujenga vyuo vya uvuvi katika
mikoa yote ambayo ina bahari ili kusaidia wananchi kupata ujuzi
kuhusiana na shughuli za uvuvi na kujipatia kipato.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha,alisema
hayo jana bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mchinga, Hamidu
Bobali, aliyetaka kujua kama serikali haioni umuhimu wa kujenga chuo
mkoani Lindi ambako kuna Bahari ya Hindi ili kuwaongezea vijana hao
ujuzi na kupata ajira.
Ole Nasha alisema Rais John Magufuli, ameonyesha nia ya dhati ya
kutaka kuwasaidia wananchi na wizara yake inatambua umuhimu wa
kuwafundisha vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za uvuvi, kilimo na
ufugaji na ndiyo maana kupitia Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi
imeanzisha Chuo cha Uvuvi Mikindani kwa lengo la kusogeza huduma ya
mafunzo ya uvuvi kwa wananchi wakiwamo vijana walioko ukanda wa kusini
mwa Tanzania ikiwemo Lindi.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment