Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti wa PIC, Richard Ndassa.
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji (PIC)
imeishauri serikali kusimamia mashirika ya umma ili kudhibiti matumizi
mabaya ya fedha ambazo serikali imewekeza katika mashirika hayo.
Akizungumza baada ya kikao cha mafunzo ya kamati hiyo na Msajili wa
Hazina jana, Mwenyekiti wa PIC, Richard Ndassa, alisema, kamati yake
ina majukumu ya kusimamia mashirika ya umma ambayo yako zaidi ya 260,
mengi yakionekena kuwa na kasoro ikiwamo matumizi makubwa kuliko mapato.
“Tumekuwa tukishuhudia mashirika mengi ya umma yanatumia fedha
nyingi katika kushughulika na masuala yasiyo na msingi kulinganisha na
mapato wanayokusanya licha ya kuwa serikali inawekeza fedha nyingi
kuendesha mashirika haya,” alisema Ndassa.
Awali, Msajili wa Hazina, Lawrance Mafuru, aliiomba kamati hiyo
kushirikiana na serikali katika kushauri namna bora ya uwekezaji katika
mashirika ya umma.
Alisema kwa kufanya hivyo, kutawezesha faida inyopatikana kuendana
na uwekezaji pamoja na kuwa na sheria madhubuti itakayoainisha usimamizi
bora wa mashirika na kuondoa mgongano wa majukumu katika usimamizi
wake.
Akiwasilisha mada kuhusu majukumu na muundo kwa ofisi ya Msajili
wa Hazina mbele ya Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Serikali, alisema
serikali imekuwa ikiwekeza pesa nyingi lakini faida inayopatikan ni
ndogo.
Alisema kiwango cha matumizi katika mashirika hayo ya umma kimekuwa
kikubwa kulinganisha na mapato ya ndani. Alisema kumekuwapo na
ongezeko la matumizi kutoka asilimia 83 mwaka 2011/2012 hadi asilimia
86 mwaka 2014/15.
Kuhusu deni la taifa, Mafuru alisema limekuwa likiongezeka kutokana
mashirika ya umma kukopa katika kuendeleza miundombinu lakini yamekuwa
yanashindwa kurudisha na kuiachia mzigo serikali.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment