Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
(Na Raymond Mushumbusi-Dodoma)
Serikali katika kuongeza
na kuimarisha uhakika na usalama wa chakula hapa nchini, Serikali
imepanga kujenga maghala 275 kwa awamu katika sehemu zenye uzalishaji
mkubwa wa zao la mahindi ambapo hadi sasa jumla ya maghala 125
yanaendelea kujengwa na kukarabatiwa katika maeneo hayo.
Akifafanua
hilo wakati akiharisha shughuli za Mkutano wa Pili wa Bunge la 11
lilikuwa na vikao 9 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema Serikali imejipanga katika kuondoa
tatizo la upungufu wa chakula nchini kwa kujenga magala mengi zaidi ya
kuhifadhi chakula katika maeneo mbalimbali yenye changamoto za upungufu
wa chakula.
Mhe.
Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema hali ya chakula kwa mwaka 2015/2016
katika maeneo mengi ya nchi imeendelea kuwa ya kuridhisha kufuatia
mavuno mazuri yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2014/2015 na takwimu za
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinaonesha kuwa albaki kutoka msimu
uliopita nchi ilikuwa na ziada ya chakula licha ya kuwepo kwa maeneo
machache ambayo hayakuwa na chakula.
“Kutokana
na uzalishaji wa mazao ya chakula kwa msimu wa 2014/2015 kuwa Tani
milioni 15.5 na mahitaji ya chakula kwa mwaka 2015/2016 kuwa Tani
milioni 12.9 hivyo nchi
imejitosheleza kwa chakula kwa ziada ya Tani milioni 2.5 sawa na
asilimia 120 na napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa Serikali
itaendelea kuhudumia maeneo yote yenye uhaba wa chakula”
“Ili
kukabiliana na hali ya uhaba wa chakula katika maeneo hayo, Serikali
inaendelea kutoa chakula katika maeneo hayo ambapo jumla ya Tani
23,871.6 za chakula zilitengwa kwa ajili hiyo na hadi
kufikia tarehe 17 Januari, 2016, jumla ya Tani 11,860.8 zilikuwa
zimechukuliwa toka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwenda
kwenye Halmashauri za Wilaya zenye upungufu wa chakula kwa ajili ya
usambazaji pia natoa wito kwa Halmashauri ambazo hazijachukua mgao wao
kufanya hivyo mara moja ili Wananchi katika maeneo hayo wasizidi
kuathirika” Alisema Mhe. Majaliwa.
Aidha, Mhe Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema
Serikali kwa kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA)
inaendelea kujenga maghala ya kimkakati kwa ajili ya kuhifadhi akiba ya
Taifa na Kwa sasa ghala moja lenye uwezo wa kuhifadhi Tani 5,000 limeshajengwa
Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya na Serikali imepata mkopo wenye masharti
nafuu kutoka Serikali ya Poland ambao utawezesha kujenga vihenge vya
kisasa (silos) vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani 160,000 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi Tani 90.
Ameongeza
kuwa Pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali, amewataka viongozi wa
Mikoa, Wilaya na watendaji katika Halmashauri zote Nchini kuwahamasisha
Wananchi kutumia vizuri mvua zinazonyesha nchini kote kwa kulima kwa
bidii ili kuweza kuvuna na kujiwekea akiba ya chakula cha kutosha kwa
ajili ya kaya zao wakati wote wa mwaka na wawahamasishe wafanyabiashara
na wadau wengine kusaidia Serikali kuchukua chakula kutoka maeneo yenye
ziada na kupeleka katika maeneo yenye upungufu na kwa kuzingatia
maelekezo haya pamoja na juhudi za Serikali zilizooneshwa, tatizo la
uhaba wa chakula nchini litapungua, kama siyo kumalizika kabisa.
Waziri
Mkuu Mhe Kassim Majaliwa,Majaliwa amehairisha Mkutano wa Pili Bunge
amehairisha shughuli za Bunge mpaka tarehe 19 mwezi April 2016 saa 3
Asubuhi likaporejea katika Mkutano wa kujadili Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017.
0 comments:
Post a Comment