Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.
Serikali imesema uamuzi wa kuyataka mashirika ya
umma pamoja na taasisi za serikali kufungua akaunti Benki Kuu (BoT)
itasaidia kupunguza riba kwenye benki.
Akizungumza bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge
wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, Waziri wa Fedha, Dk. Philip
Mpango, alisema serikali kupitia Benki Kuu itaendelea kusimamia sekta ya
fedha ili kuhakikisha riba zinapungua kwenye mabenki.
Alisema katika mapendekezo ya mpango waliouwasilisha, moja ya hatua
ambazo serikali inachukua ni kuhakikisha taasisi za umma zinafungua
akaunti katika Benki Kuu.
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha fedha nyingi
zilizokuwa zinatumiwa na mabenki kwa ajili ya kufanya biashara bila
serikali kupata faida sasa zinatumika ili mabenki hayo yaende vijijini
kupeka huduma kwa wananchi.
“Hii ni hatua moja wapo ya kusaidia kupunguza riba ili wananchi wetu waweze kunufaika zaidi,” alisema.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment