Home » » SHERIA KUBADILISHWA KUPUNGUZA MISAMAHA YA KODI.

SHERIA KUBADILISHWA KUPUNGUZA MISAMAHA YA KODI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
achague
SERIKALI imesema itaendelea kufanya mabadiliko katika sheria ili kupunguza misamaha ya kodi.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema hayo bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema) ambaye alitaka kujua serikali inachukua hatua gani ili kuondokana na misamaha ya kodi inayotolewa kwa kampuni za uwekezaji.
Alisema serikali inaendelea kufanya mabadiliko katika sheria hiyo ili kupunguza misamaha ya kodi inayotolewa kwa ridhaa, yaani misamaha inayotolewa kwa kampuni moja moja kwa mikataba na kwa kupitia katika mamlaka ya waziri wa fedha na mipango.
Alisema ili kuboresha kivutio cha msamaha kwa wawekezaji kodi imekuwa ikipunguzwa katika bidhaa na shughuli za jumla. Pia misamaha ya kodi ni moja ya vivutio vinavyotolewa kama moja ya njia ya kuwahamasisha wawekezaji ili waTanzania badala ya kwenda nchi nyingine.
CHANZO : HABARI LEO.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa