Serikali imesema wahudumu wa afya ambao bado wanatoa lugha chafu kwa
wagonjwa watafikishwa katika mabaraza ya wauuguzi na phamasia ambapo ili
kutoa maamuzi ikiwemo kuwafikisha mahakamani pale itakapobainika makosa
ni makubwa kwa wahudumu hao.
Hayo yamesemwa Bungeni Dodoma katika kikao cha Bunge ambapo Naibu
waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Khamis Kigwangalla alipokuwa akijibu swali la
Mbunge wa Viti maalum CCM Faida Mohamed Bakari.
Mbunge Farida ametaka kujua namna serikali ilivyojipanga kutokomeza
tabia mbaya ya wahudumu wa afya hasa kutoa lugha chafu kwa wagonjwa
hususani kwa kinamama wajawazito.
''Ni marufuku kwa wauguzi kutoa lugha chafu kwa wagonjwa na wana bodi
zao za taaluma zao hivyo kila mgonjwa anaehudumiwa aangalie anahudumiwa
na nani na atoe maoni yake katika eneo husika ili sheria ichukue
mtandao wake''Amesisitiza Dkt.Kigwangalla.
Dkt.Kigwangalla amesema wizara yake pia imeandaa utaratibu maalumu wa
kutoa semina kwa wakunga wa jadi ili waweze kutoa huduma vijijini kwa
utaratibu utakao leta tija zaidi.
0 comments:
Post a Comment