Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.
Baada ya serikali kukwama kuwasilisha bungeni
mapendekezo ya mwelekeo wa mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano
2016/17-2020/21, jana iliwasilisha mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti
ya serikali kwa mwaka 2016/17, jambo ambalo lilizua taharuki kwa mara
nyingine.
Kabla Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, kusoma mwongozo
huo, wabunge wa upinzani wakiongozwa na Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu na wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, walisimama kuomba mwongozo
wa kiti.
Kwa upande wake, Lissu alisema kanuni ya 94 (1) inasema katika
mkutano wake wa Oktoba na Novemba kila mwaka, Bunge kwa siku
zisizopungua tano litakaa kama kamati ya mipango ili kukidhi matakwa ya
sheria ibara ya 63(3)(C) ya katiba inayotaka kujadili mpango wa muda
mrefu au mfupi na kuutungia sheria.
Lissu pia alitumia kanuni ya 97 (1) inasema “Tarehe 11 ya mwezi wa
tatu kila mwaka na tarehe nyingine inayofuata ambayo itakuwa sio siku ya
kazi, waziri anayehusika na masuala ya mipango atawasilisha kwa wabunge
mapendekezo ya serikali ya mpango kwa mwaka,” alisema na kuongeza:
katika orodha ya shughuli za leo kuna kitu kimeletwa hapa
mapendekezo ya mpango wa taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali
katika mwaka wa fedha 2016/17, kanuni ya 94 inasema tupate mapendekezo
ya utekelezaji wa mpango sio mapendezo ya mpango ni mapendekezo ya
utekelezaji wa mpango na ibara ya 63(3)(c)inasema tupate mpango wenyewe.
Mheshimiwa Spika wewe ni mzoefu wa bunge hili, mwaka 2011
tuliletewa mpango wa taifa wa mwaka mmoja na mwaka 2014/15 tuliletewa
mpango wa maendeleo ya taifa wa mwaka mmoja leo 2016/17 tumeletewa
mapendekezo ya mwelekeo wa mpango wa maendeleo ya Taifa 2016/17.
Hichi kitu hakipo kwa mujibu wa katiba ambayo inasema kujadili na
kuidhinisha mpango na kuutungia sheria, hichi kitu kinacholetwa
hakilingani na kanuni kwasababu kanuni ya 94 inasema utekelezaji wa
mpango maana yake lazima kuwe na mpango, tulipaswa tuwe na kitu kama
hiki, hii kitu haijawahi kuletwa kwenye bunge hili, haipo kwenye kanuni
wala kwenye katiba,” alisema Lissu.
CHANZO ; NIPASHE.
0 comments:
Post a Comment