Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Dk. Abdallah Possi.
Wananchi wametakiwa kutoa taarifa dhidi ya askari
ambao wanadaiwa kuwafumbia macho wanaojihusisha na biashara za dawa ya
kulevya ili wachukuliwe hatua.
Wito huo ulitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Dk. Abdallah
Possi, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum,
Mwantumu Haji, aliyehoji ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya askari
ambao wanafumbia macho wauza dawa za kulevya.
Haji alisema kuna askari ambao hawaendani na kasi ya kuthibiti dawa
za kulevya na kuhoji ni mbinu gani zinazotumika kuthibiti tatizo hilo.
Dk. Possi alisema askari kutochukua hatua shidi ya watu
wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ni kinyume cha sheria na
kufanya hivyo ni kosa la jinai.
“Kwa wale ambao wanawafahamu askari wanaojihusisha na suala hili watoe taarifa ili wachukuliwe hatua,” alisema.
Aidha, akijibu swali la msingi la mbunge huyo, aliyehoji serikali
imejipanga vipi kunusuru vijana katika janga la utumiaji wa dawa za
kulevya, Dk. Posi alisema serikali inatambua maumizi ya dawa za kulevya
yana madhara mengi kwa watumiaji, familia na jamii kwa jumla, hivyo
imejipanga kupambana na tatizo hilo.
Alisema ili kuwanusuru vijana serikali imechukua hatua kwa kuongeza
juhudi za kimkakati za kuhakikisha wote wanaojihusisha na biashara hiyo
haramu wanakamatwa na kuadhibiwa vikali.
Alisema serikali pia inaendelea kutoa matibabu kwa watumiaji wa
dawa za kulevya katika hospitali na vituo vya magonjwa ya akili nchini
ili kuwasaidia watumiaji wa dawa hizo kuacha.
CHANZO:
NIPASHE.
0 comments:
Post a Comment