Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga amewataka maofisa
Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini kufanya kazi kwa uzalendo
ili Tanzania iweze kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) ifikapo
mwaka 2030 kama ilivyokusudiwa.
Kauli
hiyo aliitoa mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa warsha ya malengo
endelevu kwa maafisa hao kutoka kanda ya Ziwa ambayo imeandaliwa na
Wizara ya Fedha na Mipango .
Alisema
uhamasishaji kuhusu malengo haya ni matokeo ya Nchi wanachama wa Umoja
wa Mataifa kukamilisha utekelezaji wa Malengo ya Milenia yaliyokamilika
mwaka 2015.
Alisema
Mpango wa maendeleo endelevu utatekelezwa kati ya mwaka 2015 hadi 2030,
hivyo pia na unajulikana kama agenda 2030 na Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa pia iliridhia utekelezaji
wa malengo hayo.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Fedha na Mipango, Servus Sagday akielezea madhumuni ya
warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa
Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini iliyofadhiliwa na Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi kufungua warsha hiyo inayoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa
mikutano Hazina ndogo.
Alisema katika utekelezaji wa mpango huo lazima maafisa hao wawe na uzalendo kwa kufanya kazi kwa maadili.
“Bila
kubadili fikra zao malengo hayo hayataweza kufikiwa, tufanye kazi kwa
bidii ili ifikapo mwaka 2030 tuweze kujipima na kuweza
kushangilia kwa kufikia malengo ya maendeleo endelevu 17 ambayo yamejikita kwenye sekta mbalimbali,”alisema Mmbaga.
Alisema
changamoto iliyopo kwasasa ni namna ya kufikia malengo hayo, hivyo ni
lazima kuwa tayari kubadilika katika kufanya kazi na kutafsiri mambo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga akifungua warsha
ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa
Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini inayoendelea katika ukumbi
wa mikutano Hazina ndogo mjini Dodoma chini ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
“Tutakuwa
tunavutana, tunaangushana na itatupotezea muda wa kufikia kwenye
malengo haya lakini kikubwa ni lazima tukubali malengo ni ya kwetu na
yapo kwa ajili yetu sisi wenyewe ili mwisho wa siku tuweze
kuyafikia,”alisema.
Aliwahimiza
kuwa na moyo wa uzalendo ili kufikia malengo hayo katika utatuzi wa
changamoto mbalimbali zilizopo ikiwemo miundombinu.
“Lazima
tutambue watumishi wa umma ni jeshi ambalo linatakiwa kupigana na
maadui wale ambao wanatuathiri kijamii na kiuchumi na tuna maadui watatu
ujinga, maradhi na umaskini, wakati wanapopigana na maadui waliopo
kwenye malengo hayo na sisi tuunganishe na hawa maadui watatu,”alisema.
Alisema
inawezekana ikapangwa mipango mbalimbali lakini kama hawatabadili fikra
zao na hawapo tayari kufanya kazi ili kufikia malengo hayo kazi itakuwa
ni ngumu.
Alibainisha
tayari miongozo ya bajeti imeshatumwa kwenye mikoa hivyo kwa mujibu wa
miongozo hiyo waangalie namna ya kupanga shughuli, miradi ambayo
itajikita kufikia maelngo endelevu 17 ya Kitaifa na kidunia.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) -Idara ya Uchumi, Dr. Wilhelm
Ngasamiaku akitoa mada kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) na
mchakato wake katika warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDG's) kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango
nchini inayoendelea katika ukumbi wa mikutano Hazina ndogo mjini Dodoma
chini ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkufunzi
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi, Dr. Joel
Silas akitoa mada kuhusu uhusiano wa Maendeleo Endelevu (SDG's) na
mpango wa maendeleo wa miaka mitano kwenye warsha ya siku tatu ya
Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii na
Maofisa Mipango nchini inayoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa
mikutano Hazina ndogo chini ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP).
Afisa
kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Eva Ruhago
akifafanua jambo kwa washiriki wa warsha ya siku tatu ya Malengo ya
Maendeleo Endelevu (SDG's) inayoendelea katika ukumbi wa Hazina ndogo
mjini Dodoma chini ya ufadhili wa UNDP.
Pichani
juu na chini sehemu ya washiriki wakitoa maoni wakati wa majadiliano
katika warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa
Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini inayoendelea mjini
Dodoma katika ukumbi wa mikutano Hazina ndogo chini ufadhili wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Pichani
juu na chini ni sehemu ya Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango
kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mikoa ya Kagera, Kigoma, Mara,
Geita, Simiyu, Shinyanga na Mwanza wanaoishiriki warsha hiyo ya siku
tatu yenye lengo la kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi ili kutimiza
kaulimbiu ya Malengo hayo isemayo "Hakuna atakayeachwa nyuma" inayolenga
kujenga msingi wa malengo shirikishi yanayodhamiria kuleta maendeleo
chanya kwa wote.
Mgeni
rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga
(walioketi katikati) katika picha ya pamoja na Maofisa Maendeleo ya
Jamii na Maofisa Mipango kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mikoa ya
Kagera, Kigoma, Mara, Geita, Simiyu, Shinyanga na Mwanza wanaoshiriki
warsha hiyo ya siku tatu inayoendelea mjini Dodoma chini ufadhili wa
UNDP
0 comments:
Post a Comment