Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Wizara ya Fedha na
Mipango, imezindua zoezi la uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara
hiyo. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
mkoani Dodoma.
Lengo la kufanyika kwa zoezi hili ni kuhuisha
orodha ya malipo ya Wastaafu kwa mara ya mwisho zoezi hilo lilifanyika mwaka
2014.
Akizungumza wakati
wa uzinduzi wa zoezi hilo, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Mkaguzi wa Ndani
Mkuu wa Serikali Msaidizi, Stanslaus Mpembe, alisema kuwa zoezi hilo
litafanyika kwa muda wa siku tano katika Kanda ya Kati ambayo imejumuisha mikoa
mitatu ya Morogoro, Dodoma na Singida.
Mpembe alisema
lengo la kufanyika kwa zoezi hilo ni kubaini mabadiliko ya taarifa za Wastaafu
kama vile kufariki ili kuepuka kulipa Wasiostahili.
‘Zoezi hili
linafanyika kutokana na utaratibu uliojiwekea Wizara kufanya uhakiki wa
Wastaafu baada ya muda fulani, zoezi hili litafanyika nchi nzima. Mpembe
alisema’
Aliongeza kuwa
zoezi hilo litaisaidia Serikali kuhakikisha Wastaafu wote wanapata haki zao na
kwa wakati.
Aidha alitoa wito
kwa Wastaafu kujitokeza kwa wingi kuhakikiwa ili waweze kupata haki zao za
msingi, bila kusahau viambatanisho wanavyotakiwa kuwa navyo ili kurahisisha
zoezi hilo.
Naye Katibu wa
Chama Cha Wastaafu wa Mkoa wa Dodoma John Kanyeto aliishukuru Serikali kwa
kuwajali na kukubali ombi lao kuhusani Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Ashatu Kijaji kwa kufikisha ombi lao
walipofanya nae kikao la kulipwa mafao yao kila mwezi badala ya kila baada ya miezi
mitatu.
‘Niwaombe Wastaafu
wenzangu wajitokeze kwa wingi kwani zoezi hilo ni la kwa faida yao. Kanyeto
aliongeza’.
Kwa upande wa
mstaafu Bi. Halima Matonya alisema kuwa zoezi hilo limeenda vizuri na
ameipongeza Serikali kwa kuwajali na kuwakumbuka, na amewapongeza pia Waratibu wa zoezi hilo kwa kujipanga vema
na kutoa maelekezo vizuri hivyo kufanya zoezi hilo kuchukua muda mchache.
Tayari zoezi kama
hilo la uhakiki wa wastaafumwanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango
limefanyika katika Kanda za Pwani na Nyanda za Juu Kusini ambapo ilijumlisha
mkoa wa Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Katavi, Ruvuma, na Songwe.
Baada ya kukamilika
kwa zoezi hilo kanda ya kati, zoezi hilo litaendelea katika Kanda ya Kaskazini ambapo litajumuisha Mkoa wa Kilimanjaro, Arusha, Manyara na
Tanga.
0 comments:
Post a Comment