WAZIRI MHAGAMA:
KAMILISHENI UKARABATI WA NYUMBA ZA WATUMISHI MWISHO WA MWEZI HUU.
Na Daudi
Manongi-MANONGI
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Mhe.Jenista Mhagama
amemwagiza mkandarasi anayesimamia ukarabati wa nyumba watakazo ishi watumishi
wake kukabidhi nyumba hizo ifikapo tarehe 28 Mwezi huu.
Ameyasema hayo wakati
akikagua ukarabati wa makazi ya watumishi
wake yaliyopo eneo la kikuyu mkoani Dodoma yanayosimamamiwa na Mamlaka ya
Ustawishaji wa makao makuu Dodoma(CDA).
“Kama wote mnakumbuka
agizo la mheshimiwa Waziri mkuu kwamba kufikia mwezi Februari mwakani Mawaziri
wote,Manaibu Waziri,Makatibu wakuu na Manaibu wake pamoja na sehemu ya
watumishi wachache wa kila wizara lazima wawe wameshafika Dodoma na leo tupo
hapa kuhakikisha miundombinu iko sawa tayari kwa kazi ambayo tunataka kuifanya
tukiwa hapa Dodoma,”Alisema Mhe.Mhagama
Aidha amesema kuwa
nyumba hizo zimefikia katika hatua nzuri sana na hivyo ikifika februari wataanza
kuhamia kama ilivyoagizwa.
Pia Waziri Mhagama
amesema kuwa Ujenzi wa makazi ya Waziri Mkuu pia yamefikia hatua nzuri ambapo
kwa sasa wanakamilisha uwekwaji wa tenki la maji ambalo litasaidia kuhifadhi
lita laki mbili kwa siku kwa ajili ya matumizi ya kila siku na pia ujenzi wa barabara mbili
zinazofika Ofisi ya Waziri Mkuu mkandarasi ameshakamilisha ujenzi wa barabara
hizo tayari kwa matumizi.
Mhe.Mhagama
amewahakikishia watanzania na Serikali kwa Ujumla kuwa kufikia Mwezi Februari
watahamia Dodoma ili kukamilisha agizo la rais wetu wa awamu ya tano na pia
kukamilisha ndoto ya mwalimu Nyerere ya kuihamisha Serikali Dodoma.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment