Judith Mhina
- MAELEZO
·
SERA YA VIWANDA ITATUKOMBOA
Katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika Idara ya
Habari - MAELEZO ilipata fursa ya
kufanya mahojiano na Mwanasiasa na mwana Diplomasia Balozi Christopher
Liundi kuhusiana na maadhimisho hayo. Yafuatayo
ni maswali na majibu katika mahojiano hayo:
SWALI: Mheshimiwa Balozi Tanzania imetimiza
miaka 55 ya Uhuru una lipi la kuwaeleza Watanzania?
JIBU: Kwa mtazamo wangu nina mambo matatu
muhimu ninayoayaona katika hii miaka 55 ya Uhuru. Jambo la kwanza lazima
tutambue na tuone fahari kwa nchi yetu kufikisha miaka 55, bila kuwepo na machafuko
yalliyosababisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Katika miaka 55 tumeweza
kujitawala kwa amani na utulivu kutokana na viongozi wetu kuwa na busara na
kutongangania madaraka kama ilivyo kwa nchi nyingine barani Afrika.
Pili, tumeweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo katika nyanja
mbalimbali kama vile elimu, afya, miundombinu , uchukuzi na viwanda. Katika
elimu kwa mfano wakati wa ukoloni kulikuwa na shule za Wazungu, Wahindi na
Waafrika lakini sasa, watoto wote wanasoma bila kujali kama ni Mzungu Mhindi au
Mwafrika.
Mwisho, nakumbuka mara baada ya Uhuru tukaja na sheria zetu,
baraza letu la mawaziri na maamuzi yetu wenyewe. Misingi hiyo tumeidumisha na
kuridhisha kwa vizazi vya sasa na vizazi
vijavyo Yapo mambo mengi ambayo tunaweza kukumbuka ambayo hayakuwa mazuri
lakini la muhimu ni lazima ukisema uhuru umkumbuke Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage. Nyerere ambaye alitumia muda wake wote, uwezo
wake wote pamoja na waasisi wa TANU kuhakikisha nchi hii inakuwa huru.
SWALI: Mheshimiwa Balozi wewe ni kati ya
watu waliobobea katika siasa na Diplomasia za nchi na umefanya kazi na Hayati
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Unadhani muelekeo tulionao
mpaka sasa unaleta hali halisi ya nchi huru katika miaka 55 ya Uhuru?
JIBU: Muelekeo ni mzuri tena madhubuti. Umeleta
matumaini makubwa mno kutokana na kuweza kuendelea na Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, lakini pia huduma zinazotolewa na serikali yetu kwa wananchi kukua,
kuimarika na kuboreshwa zaidi.
Pili kuna hali ya amani inayowafanya watu washiriki katika
kujenga uchumi na kujiletea maendeleo. Mfano kuweka
miundombinu ili kukuza uchumi ambapo barabara zimejengwa nchi nzima kwa
kuunganisha Mikoa na Mkioa, Wilaya na Wilaya na sasa tunaelekea kuunganisha Tarafa
Kata na hatimaye vijiji. Hii ni dalili nzuri ya maendeleo na kukua kwa uchumi.
Tatu , kuongezeka kwa wataalam wetu wenyewe katika taaluma
mbalimbali ambapo wakati tunapata uhuru tulikuwa
na wataalamu wachache sana, sina takwimu lakini sasa Mtanzania anaweza kuongoza meli,
ndege, kuchimba madini na kutengeneza
barabara. Nani alitegemea Mtanzania atatengeneza barabara hapa nchini? Nani
alidhani mtanzania anaweza kurusha ndege? Nani alidhani Mtanzania naweza kuchora mchoro wa majengo marefu
tuliyonayo hivi leo.
Haya yote yanaonyesha kwamba muelekeo wetu unaleta matumaini na uko sahihi. Tumpe Mheshimiwa Rais wetu wa
Awamu ya Tano ushirikiano ili aweze kutimiza ndoto zetu.
SWALI: NIni maoni yako kuhusu nchi muelekeo
wa nchi kwenye uchumi wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa?
JIBU: Tukubali kuwa uchumi ndio msingi wa maendeleo
wa Taifa lolote. Sera zinazoandaliwa ni lazima zilenge katika kuleta maendeleo
ya nchi kiuchumi. Rais anaposema anataka
Taifa liondokane na umasikinini ni kweli tutaondokana nao, kama tutakuwa na
viwanda vidogo vya kati na vikubwa. Kutokana na viwanda watu watapata ajira
Wakulima watapata sokola uhakika la mazao yao na bidhaa zitakazozalishwa
zitauzwa ndani na nje ya nchi kwa kuwa zimeongezewa dhamani.
Watanzania tumekuwa na tatizo la kuthamini vitu vinavyotoka
nje. Mfano mzuri ni China ambao viwanda vyao vilianza kuzalisha bidhaa
ambazo zilitumika nchini mwao hadi kujitosheleza. Hivi sasa nchi hiyo imepata
soko kubwa la nje na uchumi wake umeendelea kukua.
SWALI : Suala la nidhamu kwa Watumishi wa
Umma, Taasisi, Mashirika na Idara za Serikali mara baada ya Uhuru na sasa miaka
55 ya Uhuru?
JIBU: Nidhamu ni suala la msingi mahali popote na sio mahali pa
kazi tu hata nyumbani kwako. Watanzania walizoea kufanya kazi kwa mazoea na
hivyo kukosa nidhamu. Utendaji kazi mzuri unatokana na nidhamu ambayo inamfanya
mtu afanye kazi kwa uadilifu.
Nidhamu katika Utumishi wa Umma inayosisistizwa na Rais wetu
Dkt John Pombe Magufuli Itaongeza bidii ya kazi kwa wafanyakazi viwandani na
hivyo kuongeza uzalishaji. Enzi za Baba wa Taifa Wafanyakazi na Wakulima wote
walikuwa na nidhamu na uwajibikaji
ulikuwa mkubwa zaidi ndi maana uchumi wa nchi ulikuwa wa juu. Kila mtu
aliwajibika mahali pake pa kazi.
Enzi za Baba wa Taifa unapokwenda popote duniani, ukisema
niketoka Tanzania kila mtu anajua Mtanzania ni mkweli, muwazi na ana nidhamu ya hali ya juu. Mtanzania
hawezi kupokea wala kutoa rushwa, hashiriki kwenye masuala yoyote ya kuiharibia
heshima nchi yake, mwenye kutumia madaraka yake vizuri, na asiyefuja mali ya
umma.
SWALI:: Msaada gani unaweza kumpa Mhe Rais
katika vita dhidi ya wakwepaji kulipa Ushuru?
JIBU: Kwanza namshukuru sana Rais katika suala zima la ukusanyaji kodi kwani
ameonyesha umuhimu kwa kulipa kodi
Pili,
nampongeza kwa kuanzisha mfumo unaomtaka kila mfanyabiashara kuwa na mashine za
kulipa kodi. “Mpaka sasa imefikia mahali nchi nyingine za nje wameanza kuiga
utendaji wa kazi wa Rais wetu hili ni jambo la kujivunia”. Hivyo tumuunge mkono
katika hii vita ya ukusanyaji kodi. Watanzania
wakubali mpaka sasa kwamba hatua alizochukua Mheshimiwa Rais za kukusanya kodi
ni sahihi na tuziunge mkono.
Tatu,
Serikali haina namna itakayoweza kupata fedha za kusaidia watu wake kupata
huduma za msingi. Fedha zinazokusanywa ndio zinazotumika kwenye barabara,
kununulia madawa kujenga Hospital na mabo kama hayo.
SWALI :Unaposikia siku ya Uhuru wa
Tanganyika unakumbuka nini?
JIBU: Hii inanikumbusha kauli ya Mwalimu
Nyerere alisema: “UHURU NA KAZI”, ni kweli kabisa lazima tufanye kazi kama
anavyosisitiza Rais wetu Magufuli “HAPA
KAZI TU”. Maendeleo hayaji kwa kupiga hadithi ni lazima watu wafanye kazi na
asiyefanya kazi na asile.
Pili siku hii ya Uhuru inanikumbusha juu ya elimu ambayo
wakati huo inatolewa bure, lakini baadaye ilisitishwa na kuwafanya vijana wengi
kukosa fursa ya kuendelea na masomo . Rais wetu ameamua elimu sasa itolewe bure
kuanzia shule za msingi hadi sekondari ili kuwaondolea mizigo wazazi ambao
walishindwa kuwasomesha watoto wao kutokana na gharama kubwa.
SWALI: Una wito gani kwa Watanzania katika
kusheherekea miaka 55 ya Uhuru?
JIBU: Wito wangu kwa Watanzania tusikilize
maelekezo yanayotolewa na serikali yetu ambayo ni sikivu, tuisipende kusikiliza
maneno ambayo sio rasmi na kujiamulia jambo bila kufuata sheria.Watanzania
tufanye kazi tuache uvivu tusipende kulaumu serikali wakati sisi wenyewe
tunakaa tu bila kufanya kazi. Tuunge mkono Serikali yetu kwa kila jambo
inayoelekeza kufanya.
Waandishi wa Habari wanafanya kazi nzuri sana ya kuelimisha.
Napenda kuwapongeza kwa hilo. Waaendelee kuelimisha jamii kwa kuelezea masuala
ya msingi na muhimu katika maendeleo yao na hasa nchi kwa ujumla.
Mwisho tuendelee kulinda Muungano wetu Amani yetu, Upendo,
Umoja na Mshikamano.
- MWISHO
BALOZI LIUNDI –
“NIDHAMU KATIKA UTUMISHI YAIPAISHA TANZANIA KIMATAIFA”
Judith Mhina - MAELEZO
Nidhamu katika Utumishi wa Umma inayosisistizwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Imeiweka Tanzania
katika ramani ya dunia.
Hayo yamesemwa na Balozi Christopher Liundi katika mahojiano
kwa njia ya simu yaliyofanyika wiki hii.
Mheshimiwa Balozi
Liundi alisema; Rais wetu ameweza kurejesha heshima ya Tanzania duniani
kutokana na nidhamu katika Utumishi wa Umma , ambapo heshima hiyo ilikuwepo
katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, Rais
Magufuli anaifufua ile ari na
kurejesha heshima iliyokuwepo hapo awali ;
Balozi Liundi ameeleza kwamba nidhamu katika kila kitu ni
jambo la msingi sana, iwe katika utumishi wa Umma au wa Sekta binafsi,
barabarani, hata nyumbani kwako. Nidhamu
inatakiwa itoke moyoni mwako na ufurahie hali ya kuwa na nidhamu. Nidhamu
katika Utumishi wa Umma ni lazima ni msingi kwa vijana wetu katika kupata ajira
bila ya malamiko kutokana na Waajiri na wadau wengine kuwa vijana hawafanyi
kazi au wavivu, hawana nidhamu, na viwango.
Akitoa ufafanuzi Balozi Liundi alisema, “Enzi za Baba wa
Taifa unapokwenda popote duniani, ukisema niketoka Tanzania kila mtu anajua
Mtanzania ni mkweli, muwazi na ana
nidhamu ya hali ya juu. Mtanzania hawezi kupokea wala kutoa rushwa, hashiriki
kwenye masuala yoyote ya kuiharibia heshima nchi yake, mwenye kutumia madaraka
yake vizuri, na asiyefuja mali ya umma”.
Amesema wakati umefika kwa Watanzania kumuunga mkono Rais
wetu katika kuhakikisha kwamba nidhamu katika utumishi wa Umma inakuwepo
Akiongea kuhusu miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika Balozi Liundi
amesema kauli ya Rais Magufuli la kutaka Taifa liondokane na umasikinini kwa
kufufua au kujenga viwanda vidogo vya kati na vikubwani lazima utekelezwe.
Balozi Liundi amempongeza Rais kwa jitihada zake za kuwaweka
katika utayari wafanyabiashara binafsi wa Tanzania katika kujenga viwanda.
Akiongea na wananchi alipokwenda kufungua kiwanda cha matunda cha Azam cha
Salim Said Bahkresa atahakikisha changamoto zilizopo kama umeme kwa kuagiza
TANESCO wamfungie umeme na kumpa shamba la hekari 1000 bure ili kupanda miwa
kwa ajili ya kuzalisha sukari. “Kazi ya Serikali ni kuweka mazingira mazuri ya
uwekezaji ambao kwa vitendo Rais amelithibitisha hili”.
Pia
nampongeza kwa kuanzisha mfumo unaomtaka kila mfanyabiashara kuwa na mashine za
kulipa kodi: “Mpaka sasa imefikia mahali nchi nyingine za nje wameanza kuiga
utendaji wa kazi wa Rais wetu hili ni jambo la kujivunia”. Hivyo tumuunge mkono
katika hii vita ya ukusanyaji kodi.
Tunapoadhimisha miaka 55 ya Uhuru wetu tukumbuke kauli ya
Mwalimu Nyerere alisema: “ UHURU NA
KAZI”, ni kweli kabisa lazima tufanye kazi kama anavyosisitiza Rais wetu Magufuli “HAPA KAZI TU”. Maendeleo hayaji kwa
kupiga hadithi ni lazima watu wafanye kazi na asiyefanya kazi na asile. –
MWISHO -
0 comments:
Post a Comment