Benjamin Sawe
Maelezo
Mkuu
wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma Bw. Deogratius Ndejembi amepiga marufuku
matumizi ya nafaka kutengenezea pombe za kienyeji ili kujikinga na baa la njaa.
Bw.
Ndejembi amesema kumekuwa na tabia ya wananchi kufanya sherehe zisizokuwa na
tija ikiwemo zile za jando na ngoma za asili kwa kutumia nafaka
Akizungumza
na Idara ya Habari Bw. Ndejembi amesema hivi sasa wilayani Kongwa kipo
chakula cha kutosha majumbani, sokoni na kwenye Maghala yanayotumika kuhifadhi
chakula.
Amesema
chakula kilichopo kikitumika vizuri kitawatosheleza wananchi mpaka pale
watakapovuna mazao mengine katika msimu wa mavuno ujao.
“Kongwa
chakula kipo cha kutosha, wanaosema hakuna chakula ni wafanyabiashara wanaotaka
kuzua hofu ili wapandishe bei ya mazao na wanasiasa waliokosa ajenda” Alisema
Ndejembi.
Mkuu
huyo wa wilaya amesema hakuna sababu ya kuficha kama itatokea kuna upungufu wa
chakula lakini kwa sasa hakuna upungufu wowote wa chakula wilayani Kongwa.
Bw.
Ndejembi amefanya ziara ya kutembelea maghala ya chakula yaliyopo Kibaigwa
wilayani Kongwa ambako pia kuna soko la mahindi la kimataifa na kujiridhisha na
chakula kilichopo.
“Mahindi
yapo ya kutosha na kama unavyojua hili ni soko la Kimataifa inamaana kungekuwa
na upungufu ungeanzia hapa” Alisema Ndejembi.
0 comments:
Post a Comment