Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepisha Muswada
wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016 (The Legal Aid
Bill, 2016).
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akitoa
taarifa wakati wa kuwasilisha muswada huo amesema kuwa muswada huo wa
sheria umepitia hatua nyingi na umechukua muda mrefu hadi kufikia hatua
ya kujadiliwa na Bunge tukufu.
Aliendelea
kwa kusema kuwa muswada huo unapendekeza kutungwa kwa sheria ya msaada
wa kisheria kwa lengo la kuanzisha (kwa mara ya kwanza katika histori ya
nchi) mfumo wa kisheria wa kusimamia, kuratibu, kurasimisha na kutambua
utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria katika mashauri yote ya Jinai na
Madai kwa mahitaji.
Aidha
utaratibu uliokuwepo kwa miaka mingi kwa upande wa Serikali unahusu
baadhi tu ya makosa ya Jina, makosa yenye adhabu kubwa kama vile ya
kunyongwa hadi kufa na vifungo virefu. Ambapo huduma hiyo imekuwa
ikitolewa katika ngazi ya Mahakama Kuu pekee na kwa wigo mdogo tu pale
inapohitajika kwa maslahi ya haki na kwa maelekezo ya Jaji Mkuu au
yeyote aliyekasimiwa mamlaka ya kutoa maelekezo hayo.
“Kumekuwepo
na ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma ya msaada wa kisheria na
wasaidizi wa kisheria. Kutokana na hali hiyo, Serikali imeona ulazima wa
kuanzisha mfumo wa kusimamia na kuratibu utoaji wa huduma hiyo ili
kuhakikisha inatolewa na watu wenye sifa, kwa wahitaji halisi na kwa
taratibu zinazofahamika ili iendane na matakwa ya kikatiba,” alifafanua
Dkt. Mwakyembe.
Vile
vile ameeleza kuwa muswada huo unalenga kuwatambua wasaidizi wa
kisheria, kufuta sheria ya msaada wa kisheria (katika mashauri ya
Jinai).
Kwa
upande wake Mbunge Selemani Zedi amesema kuwa, muswada huo utawasaidia
wananchi ambao hawana uwezo wa kuwalipa Mawakili wanapohitaji msaada wa
Kisheria.
Aidha,
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson ameipongeza Serikali kwa muswada huo
muhimu ambao Bunge umeipitisha unasuobiria kutiwa saini na Mhe. Rais ili
kuwa Sheria.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment