Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
amewahakikishia wapenzi wa Mpira Mjini Dodoma kuwa timu za Mpira Mkoani
humo zitashiriki Ligi Kuu ili kuwapa raha ya Ligi hiyo mashabiki wa
mpira na michezo kwa ujumla.
Amezungumza
hayo mara baada ya kukutana na kufanya mazoezi na Vijana kutoka Jogging
Club mbalimbali Mjini Dodoma ikiwa ni ishara rasmi ya Wizara yake
kuhamia katika Makao Makuu ya nchi.
Mhe.
Nape Nnauye amesema kuwa haitawezekana Serikali ikahamia Dodoma na
kusiwe na timu inayoshiriki Ligi kuu ya Mpira wa Miguu Tanzania Bara
hivyo yeye kama Waziri anayehusika na Michezo kwa kushirikiana na wadau
wa Michezo atahakikisha Timu zinafanya vizuri na kushiriki Ligi hiyo.
“Haiwezekani
Rais akawa hapa na Makamu wa Rais na Mawaziri tukakosa ladha na furaha
ya Ligi kuu hapa Dodoma nitahakikisha timu za hapa zinashiriki Ligi
kuu”alisistiza Mhe. Nnauye.
Kwa upande wake Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde
amewapongeza vijana wa Jogging club na wakazi wa Dodoma kwa kushiriki
michezo na kuhimiza kujituma zaidi kwa timu za michezo hasa mpira wa
miguu ili kushiriki Ligi kuu Tanzania Bara.
Naye
Katibu Mkuu Wizara wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante
Ole Gabriel amewaomba wakazi wa Dodoma kufanya michezo kuwa ni Utamaduni
wao wa kila siku ili kujenga Taifa la wapenda michezo kwa nia ya
kuimarisha afya na kuendeleza michezo nchini.
Aidha
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini Bw. Omary Singo
amewahakikishia wakazi na wapenzi wa Michezo ushirikiano katika
kuendeleza na kukuza michezo hasa katika makao makuu ya nchi Dodoma.
0 comments:
Post a Comment