Na Mwandishi wetu- Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kuna
athari kubwa za kutotoa taarifa muhimu na za wazi zinazohitajika na
wananchi hivyo kuwanyima haki ya kujua utendaji wa Serikali.
Waziri
Nape alisema kwa sasa utoaji wa habari na taarifa za Serikali kwa umma
si utashi tena wa Afisa Habari au kiongozi wa Ofisi ya Umma bali ni
matakwa ya kisheria ambayo yamewekewa kanuni na misingi katika Sheria za
Huduma ya Habari na Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa za 2016.
“Kwa sasa kutoa habari zilizo wazi tena kwa wakati, sio utashi wa mtu tena bali ni matakwa ya Sheria hivyo ni wajibu wa kiongozi kutoa taarifa kwa umma” alisisitiza Waziri Nape.
Aidha
alisema kuna baadhi ya Maafisa Mawasiliano ambao mpaka mwaka unakwisha
hawajawahi kuandika taarifa yoyote kwa umma wala kutoa ufafanuzi kuhusu
utendaji wa Serikali hivyo kuijengea Serikali taswira mbaya kwa
Wananchi.
“Katika
awamu hii hakuna “Mungu Mtu” katika utoaji wa taarifa hivyo ni wajibu
wa viongozi kutoa taarifa au ufafanuzi pale inapohitajika na sio kukwepa
waandishi wa habari, na kutofuatilia kero za Wananchi ” alisema Waziri
Nape.
Waziri
Nape aliwataka Maafisa Mawasiliano na Viongozi katika Taasisi za umma
nchini kutekeleza Sheria ipasavyo kwa kutoa habari na taarifa kwa umma
bila urasimu.
“Ndugu
zangu msikalie taarifa maana kama hutoi ushirikiano kwa wana habari na
wote wanaohitaji taarifa watatunga zakwao ,hapo sasa mnaanza kukimbizana
kukanusha” ,Alisisitiza Waziri Nape.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment