Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi imeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana na upungufu wa maziwa nchini.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.Dk Charles Tizeba
wakati akijibu swali la Mbunge wa Wete Mhe.Mbarouk Salum Ali leo Bungeni
MJini Dodoma katika Kikao cha thelathini na sita cha bunge la 11.
“Nakubaliana
na Mhe.Mbunge kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya mifugo lakini bado kuna
upungufu wa maziwa,ambapo takwimu za makadirio za mwaka 2016
zinaonyesha lita bilioni 2.09 za maziwa zilizalishwa na unywaji wa
maziwa kwa mtu kwa mwaka ulifikia lita 47 ukilinganisha na lita 200
zinazopendekezwa na Shirika la chakula Duniani(FAO)”,Alisema Mhe.Tizeba
Aidha
kati ya Ngombe milioni 28.4, Ngombe rasmi wa maziwa ni 782,995 tu sawa
na asilimia 3 ya Ng’ombe wote.Aidha kati ya mbuzi milioni 16.7 ni mbuzi
rasmi takribani 50,000 ndio wa maziwa ambao ni asilimia 0.3 ya mbuzi
wote.
Amezitaja
jitihada ambazo Serikali imechukua ili kukabiliana na upungufu wa
maziwa nchini ni pamoja na kumarisha mashamba ya kuzalisha mifugo ya
Serikali (LMU’s) ili kuongeza idadi ya Ng’ombe wenye uwezo wa kuzalisha
maziwa kwa wingi.
Aidha
Serikali imeanzisha vituo vya uhimilishaji katika kanda 6 hapa nchini
ambazo ni kanda ya Ziwa(Mwanza),kanda ya Magharibi(katavi),Kanda ya
kati(Dodoma),Kanda ya Mashariki(Kibaha),Kanda ya Kusini(Lindi) na Kanda
ya Nyanda za Juu Kusini(Mbeya) kwa lengo la kutoa huduma ya uhilimishaji
wa Ng’ombe wa Maziwa walioko kwenye maeneo hayo pamoja na Ng’ombe wa
Asili ili kuzalisha idadi kubwa ya Ng’ombe wa Maziwa.
Amehimiza
kuwa Jitihada hizi zitawezesha idadi ya Ng’ombe wa Maziwa kufikia
milioni 2.9 ifikapo mwaka 2021/22 ambao pamoja na ng’ombe wa asili
wataweza kuzalisha lita bilioni 3.8 za maziwa.
“Serikali
inaendelea kuhamasisha sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo
kuwekeza katika uzalishaji wa mitamba ya maziwa na mashamba ya ng’ombe
wa maziwa kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa maziwa hapa
nchini”,Aliongeza Mhe.Tizeba
0 comments:
Post a Comment