Home » » WAZIRI WA KILIMO AZINDUA MWONGOZO WA KILIMO KINACHOHIMILI TABIANCHI

WAZIRI WA KILIMO AZINDUA MWONGOZO WA KILIMO KINACHOHIMILI TABIANCHI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Dk. Charles J. Tizeba (MB) amezindua Mwongozo na Wasifu wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi. Tukio hilo limefanyika katika ukumbi wa Wizara katika makao makuu mjini Dodoma.

Uzinduzi huo umefanyika wakiwepo washiriki na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiongozwa na DK. Fred Kafeero, Mwakilishi Mkazi wa FAO, Dk. Sebastian Grey, Mwakilishi wa CIAT. 

Wengine waliokuwepo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo Maji na Mazingira, Mheshimiwa Dk. Mary Nagu (MB), na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Atashasta Nditiye (MB). 

Washiriki wengine walikuwa ni wadau wa kilimo hapa nchini kama vile taasisi zisizo za kiserikali, sekta binafsi ambazo wanashirikiana na serikali katika maendeleo ya kilimo hususan kinachohimili mabadiliko ya tabianchi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa