Wadau
wa Habari nchini wakiongozwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa
Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakfu wa Taasisi
Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamefanya semina ya siku moja kwa lengo la
kuboresha mahusiano ya utendaji wa kazi iliyoshirikisha Serikali na
wadau wa habari nchini.
Semina
hiyo pia ilihudhuriwa na maafisa wa Serikali wakiongozwa na Naibu
Waiziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii Bi Annastazia Wambura,
Wabunge, wawakilishi wa vyuo vikuu, viongozi wa taasisi za Habari
nchini, wahariri na waandishi.
Naibu
Waziri, Anastazia Wambura akizungumza kwenye mkutano huo amesema
serikali iko bega kwa bega na waandishi wa habari ili kufikia malengo
waliyojiwekea katika kuhabarisha umma.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura
akizungumza kwenye mkutano wa wadau mbalimbali wa habari waliokutana
kujadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ili kuleta ustawi
wananchi leo kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Usajili wa Magazeti, Bw. Patrick
Kipangula akiwasilisha mada kuhusu sheria ya vyombo vya habari
aliyoiwasilisha kwenye mkutano wa wadau wa vyombo vya habari waliokutana
na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia
Wambura.
Mjumbe
wa Bodi ya MISA Tanzania, James Marenga akizungumza kuhusu umuhimu wa
vyombo vya habari hasa kwenye sheria ya vyombo vya habari.
Mhariri
Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akiwasilisha mada kuhusu
namna ya kufanya mahusiano ya kikazi kati ya serikali na wanahabari kwa
baadhi ya wabunge, wahariri, Maafisa habari na waandishi wa habari
katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa(kushoto)
akitolea ufafanuzi baadhi ya mambo yanayohusu Idara ya Habari Maelezo
yaliyoulizwa na wadau wa habari kwenye mkutano uliowakutanisha wadau
mbalimbali wa habari waliokutana leo kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo mjini
Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Anastazia Wambura.
Mhadhiri
Msaidizi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Paul Dotto Kuhenga
akiwasilisha mada kwa wahariri, waandishi wa habari na maafisa habari wa
Serikali waliokutana kujadili njia bora ya kufanya kazi kwa pamoja leo
kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Afisa
Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza
jambo mbele ya baadhi ya wabunge na baadhi ya wahariri, waandishi wa
habari pamoja na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari waliofika katika
semina ili kujadili jinsi ya kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya
Serikali na wanahabari yatakayoleta ukaribu kwa pande zote.
Baadhi
ya wadau mbalimbali wa vyombo vya habari wakichangia mada kuhusu namna
ya kushirikiana kati ya Serikali na vyombo vya habari hapa nchini ili
kuleta ufanisi katika tasnia ya habari.
0 comments:
Post a Comment