Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kushoto) akizungumza jana
mjini Dodoma katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia Bodi ya Utalii
Tanzania kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Kulia ni
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Albert Obama.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence
Milanzi (kushoto) akizungumza jana mjini Dodoma katika semina iliyoandaliwa na
Wizara hiyo kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe
wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu majukumu
ya bodi hiyo. Katikati ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani na Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Albert Obama.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma
(PIC), Albert Obama (kulia) akizungumza jana mjini Dodoma katika semina
iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili
ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Katikati
ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani na Katibu Mkuu, Wizara ya
Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Meneja wa Huduma za Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga (kushoto) akiwasilisha mada ya jumla kuhusu shughuli za taasisi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia bodi hiyo mjini Dodoma jana.
Meneja wa Huduma za Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga
(kushoto) akiwasilisha mada ya jumla kuhusu shughuli za taasisi hiyo kwa wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika semina
iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia bodi hiyo mjini Dodoma jana.
Meneja wa Huduma za Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga (kushoto) akiwasilisha mada ya jumla kuhusu shughuli za taasisi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia bodi hiyo mjini Dodoma jana.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiangalia video zilizoandaliwa na TTB kwa ajili ya kutambulisha utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia bodi hiyo mjini Dodoma jana.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma
(PIC) na Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Lulida akichangia jana mjini Dodoma katika
semina iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa
ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia Bodi ya Utalii Tanzania mjini Dodoma jana.
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Meena akifafanua jambo katika semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia Bodi ya Utalii kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu majukumu ya bodi hiyo.
NA HAMZA TEMBA - WMU
.................................................................................
Wizara
ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania TTB, imefanya
semina ya mafunzo ya siku moja kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kwa
lengo la kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu majukumu ya taasisi hiyo
ambayo imefanyika jana mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa
Wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani na Katibu Mkuu, Meja Jenerali Gaudence
Milanzi.
Akizungumza
katika semina hiyo, Meneja wa Huduma za Utalii wa taasisi hiyo, Philip
Chitaunga alisema bodi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1993 ilipewa jukumu la
jumla la kukuza sekta ya utalii nchini ikiwemo kutumia mbinu mbalimbali
za utangazaji, kuhamasisha uendelezaji wa mazao ya utalii na miundombinu
yake, kufanya tafiti za masoko na utalii kwa ujumla pamoja na
kuhamasisha uelewa wa watanzania kufahamu umuhimu na faida za utalii.
Alisema
taasisi hiyo imefanya juhudi mbalimbali za kutangaza utalii wa Tanzania
nje ya nchi ikiwemo kuratibu ziara za waandishi wa habari za kitalii,
kuweka matangazo katika magazeti ya utalii ya kimataifa, kushiriki
katika maonesho ya utalii ya kimataifa na kutangaza kupitia Televisheni
za kimataifa kama CNN ya Marekani.
“Jitihada
zingine tulizofanya ni kutumia balozi zetu nje ya nchi na mabalozi wa
utalii wa hiari yaani 'Goodwill Ambasadors', kutumia mitandao ya kijamii
na matangazo kwenye vyombo vya usafiri vya umma ambapo mwaka 2008 hadi
2009 tulitangaza kwenye mabasi 124 jijini london Uingereza, taxi 100,
treni mbalimbali na katika uwanja wa ndege wa Heathrow” alisema
Chitaunga.
Alisema
jitihada za hivi karibuni za kutangaza utalii zimefanyika kupitia
michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza ikiwemo timu za mpira wa miguu za
Seattle Sounders na Sunderland, kupitia majarida, CD na filamu fupi kwa
lugha mbalimbali kama Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili.
Pia, kupitia tovuti maalum ya utalii ya taifa (www.tanzaniatourism.gotz),
App kwenye ‘Smart Phones’ na kufanya ziara za utangazaji wa utalii
yaani Roadshows katika nchi za China, Afrika ya Kusini, bara la Ulaya,
Amerika na Australia.
Kwa
upande wa jukumu la kuhamasisha utalii wa ndani, Chitaunga alisema bodi
imetekelza jukumu hilo kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari
nchini pamoja na mitandao ya kijamii, kushiriki katika maonesho
mbalimbambali ya ndani ya nchi kama vile Sabasaba na Kili Fair,
kuhamasisha wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo, kuendesha
matangazo mbalimbali ya Radio na TV na kuweka mabango maeneo mbalimbali
ikiwemo ya mpakani na kwenye viwanja vya ndege.
Aliseme
katika kuhamasisha utalii wa ndani, siku za hivi karibu TTB imeingia
makubaliano na chama cha wenye mabasi nchini TABOA ambapo filamu
mbalimbali zinazohamasisha utalii wa ndani zitaoneshwa katika mabasi
zaidi ya 300 ya mikoani.
Akizungumzia
kuhusu mafanikio, alisema taasisi hiyo imechangia ongezeko la idadi ya
watalii wa kimataifa nchini kutoka 230,166 mwaka 1993 na kufikia
1,284,279 mwaka 2016. Aidha, mapato yameongezeka kutoka Dola za
Kimarekani Milioni 146.84 na kufikia Dola za Kimarekani Milioni 2,132
huku sekta hiyo ya utalii ikichangia asilimia 17.5 ya pato la taifa.
Alisema
mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na Tanzania kupata umaarufu
mkubwa zaidi duniani ambapo mitandao na kampuni mbalimbali za safari za
kitalii ikiwemo Safari Bookings, Fox News.com na New York Times
zimeitambua kama eneo bora la utalii barani Afrika. Aidha, Mlima
Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
zimetambuliwa kama miongoni mwa maajabu saba barani Afrika huku kampuni
ya World Travel Awards ikiutambua Mlima Kilimanjaro kama kivutio bora
zaidi barani Afrika.
“Baadhi
ya watu maarufu duniani kutembelea Tanzania kama vile Oprah Winfrey,
Bill Gates, Will Smith, Roman Abramovic, David Beckham, Moussa Sissoko
na Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel, Ehud Barak ni sehemu pia ya viashiria
vya mafanikio kwa taasisi yetu kutangaza utalii wa Tanzania nje ya
nchi”, alisema Chitaunga.
Aliongeza
kuwa, watu maarufu kuja kuandaa filamu zao Tanzania ni sehemu ya
mafanikio ya kutangaza utalii wa Tanzania nje ya nchi, “Watu mashuhuri
saba kutoka China hivi karibuni wameandaa filamu itakayorushwa katika
Anhui TV inayotazamwa na watu zaidi ya milioni 800 duniani” alisema.
Katika
jitihada za kutangaza utalii wa Tanzania kupitia shirika la ndege la
Air Tanzania Chitaunga alisema, “TTB sasa inaandaa gazeti la Air
Tanzania litakalojulikana kama Safari Njema kwa ajili ya kutangaza
utalii wa Tanzania na vivutio vyake pamoja na kuimarisha usafiri wa anga
kupitia shirika hilo la Umma”.
Alisema
pamoja na mafanikio hayo, bodi hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo miundombinu hafifu katika baadhi ya maeneo ya vivutio
vya utalii, changamoto ambayo imeanza kufanyiwa kazi na Serikali
ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, uimarishaji wa viwanja vya ndege na
kuimarisha shirika la ndege la Air Tanzania.
Alisema
changamoto nyingine ni ufinyu wa bajeti ya utangazaji, hofu ya matukio
ya ugaidi na mlipuko wa magonjwa katika bara la Afrika, upungufu wa
vyumba vya malazi katika baadhi ya maeneo yenye vivutio vya utalii,
mtazamo hasi kuwa Tanzania ni ghali na mtazamo kuwa jukumu la utangazaji
na uendelezaji utalii ni la Wizara na Taasisi zake pekee. Alisema
changamoto zote hizo zinafanyiwa kazi ikiwemo kuhamasisha wawekezaji
kuwekeza katika sekta ya utalii na watanzania kuona umuhimu wa utalii na
kuutangaza pamoja kuwatoa hofu watalii na kuwawekea mazingira bora na
rahisi ya kutembelea Tanzania.
Akizungumzia
mipango ya baadaye ya taasisi hiyo, Chitaunga alisema ni pamoja na
kutafsiri tovuti ya utalii ya Taifa katika lugha ya Kijerumani, Kichina
na Kiswahili, kuendeleza juhudi za kufungua masoko mapya ya utalii kama
vile China, Israel, Urusi na India, kuimarisha utangazaji wa utalii
kupitia TEHAMA, kuongeza idadi ya mabalozi wa hiari katika masoko
mahususi ya utalii, uwekaji wa mabango, tafiti za masoko mapya ya utalii
na kuandaa filamu mpya za kuitambulisha Tanzania ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Albert Obama aliipongeza Wizara na TTB kwa semina hiyo pamoja na
jitihada wanazozifanya za kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya
nchi na kutaka juhudi zaidi ziongezwe huku baadhi ya wabunge
waliochangia wakiitaka Serikali iongeze uwekezaji katika bajeti ya
utangazaji ili taasisi hiyo iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Naye
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani alisema ushauri
uliotolewa na wabunge hao utafanyiwa kazi na hoja zote zilizowasilishwa
zitajibiwa kwa maandishi huku Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali
Gaudence Milanzi akihitimisha kwa kusema kuwa Wizara imepiga hatua kubwa
ya kukabiliana na ujangili ndani na nje ya maeneo ya hifadhi nchini.
0 comments:
Post a Comment