Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua mashine ya
EFD na risiti ya kieletroniki aliyopewa baada ya kununua bidhaa kwenye
moja ya maduka mjini Dodoma, alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua
kama wafanyabiashara wa mji huo wanatumia ipasavyo mashine hizo.
Kiongozi
wa Timu Maalumu ya Ukaguzi wa Mashine za EFD’s kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Bw. Godfrey Patrick (wa pili kushoto)
akifafanua jambo wakati wa ziara ya kushitukiza iliyofanywa na Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), kwenye maduka mjini Dodoma.
Mfanyabiashara
wa duka la rejareja mjini Dodoma, Bw. Donald Chami, akimwonesha mashine
ya kieletroniki ambayo imeharibika, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (Mb), baada ya kufanyaziara ya kushitukiza kwenye duka
lake na kubaini kuwa hatoi risiti za kielektroniki kwa wateja wake.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akipitia kwa makini
fomu ya makadirio ya kodi iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) katika moja ya duka la vipodozi mjini Dodoma wakati alipofanya
ukaguzi wa matumizi ya mashine za EFD’s katika baadhi ya maduka yaliyopo
mjini humo.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akimuonya
mfanyabishara wa mjini Dodoma, Bw. Isdori Shirima, baada ya kukuta
akiuza bidhaa bila kutoa risiti za kielektroniki kwa wateja wake
inavyotakiwa na kuagiza Mamlaka ya Mapato mkoani humo kufanya ukaguzi wa
kina ili kubaini kiwango cha ukwepaji kodi cha mfanyabiashara huyo na
kumchukulia hatua za kisheria.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua risiti ya
mteja aliyenunua tanki la kuhifadhia maji katika moja ya duka linalouza
vifaa vya ujenzi mjini Dodoma, na kutoa wito kwa wananchi kukagua risiti
zao ili kubaini kama kiwango kilichoandikwa kinalingana na kiasi
kilichoandikwa kwenye risiti.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akimwelekeza mwananke
mmoja aliyemkuta dukani akague risiti yake baada ya kufanya manunuzi
kwenye duka moja la vifaa vya ujenzi mjini Dodoma, alipofanyaziara ya
kushitukiza ili kubaini namna wafanyabiashara wa maduka mjini humo
wanavyotumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akimuagiza Meneja
Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Bw. Ngaka
Magere, kumkutanisha na mawakala wanaosambaza mashine za kieletroniki za
kutolea risiti mkoani humo baada ya kutoridhishwa na huduma zao.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akisikiliza maelezo ya
matumizi ya mashine za kielektroniki kutoka kwa mfanyakazi wa Kituo
kimoja cha Mafuta mjini Dodoma, alipofanyaziara ya kushitukiza kituoni
hapo kuangalia matumizi ya mashine hizo.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua risiti na
kupata maelezo kutoka kwa mhudumu wa Kituo cha Mafuta cha ORYX mjini
Dodoma, Bi. Hanifa Shaldin, alipofanya ziara ya kushitukiza kuangalia
kama vituo vya mafuta mjini humo vimefungwa mashine za kielektroniki za
kutolea risiti kwa wateja wao. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-WFM).
0 comments:
Post a Comment