BENKI ya NMB imezindua rasmi siku ya walimu katika Mkoa
wa Dodoma. Uzinduzi huo wa siku ya walimu Mkoa wa Dodoma ulizinduliwa
rasmi na Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge
akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Jordan Rugimbana.
Hafla hii adhimu ilifanyika katika ukumbi wa Hazina na kuhudhuliwa na
zaidi ya walimu 200 wa mkoa huo mwishoni mwa wiki. Uzinduzi wa hafla hii
ni miongoni mwa mikakati ya NMB ya kuwafikia walimu nchini kote. Kusudi
kubwa la hafla hiyo ya NMB na Walimu ni kuwaongezea uelewa walimu juu
ya huduma za benki.
Hii ni kutokana na umuhimu wa kundi hili kubwa katika jamii
inayotuzunguka. NMB wanaimani kwamba mwalimu akielimika jamii nzima
itakua imepata elimu ya huduma za kifedha. Lakini pia kwa kuzingatia
ukubwa wa kundi hili NMB imekua ikitumia fursa hii kupokea mrejesho ya
jinsi huduma za kibenki zinavyopokelewa na wateja wake.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo mjini Dodoma, Meneja mwandamizi wa
wateja binafsi wa NMB, Omari Mtiga alisema NMB inazo huduma mbalimbali
ambazo kusudi lake kubwa ni kumsaidia mteja aweze kujikwamua kiuchumi.
Aliongeza kuwa zipo huduma za mikopo ya aina mbalimbali ambapo walimu
wanaweza kunufaika nayo.
Mikopo ambayo inatolewa na Benki ya NMB sio kwa ajili ya wafanyabiashara
tu bali ni kwa ajili ya kila mtu mwenye vigezo vya kukopeshwa ambapo
walimu ni miongoni mwa walengwa wa mikopo hii. Msichukue mkopo benki
kama hamna mipango thabiti ya matumizi ya mkopo huo, Ni vyema kuchukua
mkopo benki ukiwa na mipango endelevu," alisema Bw. Omari Mtiga.
"...Tukiwa kwenye mikakati ya serikali ya Viwanda ni vyema mkatumia
vizuri maonyesho ya Nane nane yanayotarajiwa kuanza kutembelea mabanda
ambayo mtajifunza namna ya uwekezaji kwenye sekta viwanda ili kujikwamua
kiuchumi kwa kutumia uwepo wa benki ya NMB kwenye jamii yetu bila
kuathiri mwenendo wa jaira zetu. Alisema kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Bi. Rehema Madenge katika hafla hiyo.
0 comments:
Post a Comment