Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wawakilishi wa vikundi vya vijana na kinamama wa Manispaa ya Dodoma wakipokea hundi ya Sh.Milioni 70 kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali.
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akizungumza na wajasiriamali wa Manispaa
ya Dodoma katika hafla ya kukabidhi hundi ya Sh.Milioni 70 kwa ajili ya
vikundi vya Kinamama na Vijana.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akitoa taarifa ya mikopo ya vijana
na kinamama kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani
Jafo.
Meya
wa Manispaa ya Dodoma Profesa Davis Mwamfupe akimkaribisha Nabu Waziri
Ofisi ya Rais, Selemani Jafo kuzungumza katika hafla ya kukabidhi hundi
ya Sh.Milioni 70 kwa ajili ya vikundi vya kinamama na vijana.
Mwakilishi wa kikundi cha vijana akimpongeza Naibu Waziri kwa maelekezo aliyoyatoa.
Mmoja wa kinamama wajasiriamali akitoa shukrani kwa serikali baada ya kuwezeshwa.
NAIBU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amezitaka
halmashauri kuwawezesha vijana na kinamama kwa vitendo kwa kuyapa
makundi hayo baadhi ya kazi zilizo chini ya halmashauri ambazo wanao
uwezo wa kuzifanya ili wajiongezee kipato.
Jafo
ameyasema hayo leo katika hafla ya kukabidhi hundi ya Sh. milioni 70
iliyotolewa na Manispaa ya Dodoma kwa vikundi vya ujasiliamali vya
vijana na kinamama ndani ya manispaa hiyo.
Ameeleza
kwamba haipendezi kwa halmashauri yeyote kuwanyima fursa ya kazi
vikundi vya vijana na kinamama ambapo kazi hizo zinaweza kufanywa na
makundi hayo.
Jafo
ametolea mfano kikundi cha vijana cha DOYODO ambacho kina kiwanda cha
kisasa cha kufyatua Matofali lakini wanahangaika soko la kuuzia
matofali wakati kuna ujenzi mkubwa wa madarasa na vyoo unaotarajiwa
kuanza hivi karibuni.
“Kwa
mfano kuna ujenzi unatarajia kuanza kwenye shule za msingi za Nkuhungu,
Mwenge, na Ihumwa ambapo kuna zaidi ya vyumba 12 vya madarasa na vyoo
matundu zaidi 18,”amesema
Naibu
Waziri Jafo ameipongeza manispaa hiyo kwa kuvitumia vikundi vya vijana
katika utengenezaji wa madawati ya shule za msingi na sekondari na
amezitaka halmashauri nyingine hapa nchini kuiga mfano huo.
0 comments:
Post a Comment