Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kwanza Kulia) akisalimiana na Wakina Mama wa Kijiji cha Msangambuye wakati wa Ziara yake Wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene(mbele) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msangambue, Kata ya Mtera Tarafa ya Rudi wakati wa Ziara yake Katika Jimbo la Kibakwe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene(mbele) akitoa maelekezo kwa Wazee wa Kijiji cha Msangambuye wakati wa Ziara ya Kikazi Jimboni Kibwakwe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene(mbele) akizungumza na mwanafunzi wa darasa la kwanza Yusta Mwanshinga katika shule ya Msingi Msangambuya alipopita kuwasalimia wanafunzi wa shule hiyo wakati wa ziara yake.
Mama Theresia Costantine Komba (kushoto) akimshkuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene kuwatembelea katika Kijiji cha Chinoje.
Na. Nteghenjwa Hosseah, Kibakwe.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene amewaagiza
Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini kuandaa mazingira rafiki kwa
watumishi wapya wanaopangiwa katika Halmashauri zao.
Simbachawene
ameyasema hayo ikiwa ni wiki moja tangu kutangaza ajira mpya za Walimu
wa Masomo ya Hisabati na Sayansi wapatao 3,081 wa ngazi ya Shahada na
Stashahada ambao wamepangiwa kwenye Halmashauri mbalimbali Nchini.
Akizungumza
na wananchi wa Kijiji cha Msangambuya wakati wa Ziara yake ya Kikazi
Wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe Mhe. Simbachawene amesema
watumishi wengi wapya wanakatishwa tamaa na mazingira mabovu
wanayoyakuta katika Halmashauri zao na hali hiyo huwatia hofu ya
kuendelea kukaa katika maeneo hao.
Unakuta
mtumishi anafika Halmashauri malipo yake hayajaandaliwa zaidi ya mwezi
mzima, kisha anapangiwa kwenye Kata mbayo hata hajawahi kuifahamu hapo
awali na hapewi hata maelekezo ya ziada ya namna ya kufika katika Kituo
chake na unakuta wenyeji wake katika Kata na Shule hawana taarifa za
ujio wa mtumishi huyo hivyo mtumishi anahangaika mpaka anakosa ari ya
kufanya kazi katika kituo chake kipya alisema Simbachawene.
“Ninahitaji
Kila Halmashauri kuandaa Malipo stahiki kwa ajili ya walimu
wanaoendelea kuripoti hivi sasa katika maeneo mbalimbali, Usafiri wa
kuwapeleka katika vituo vyao vya Kazi, mapokezi stahiki kwa uongozi wa
Kata pamoja Shule sambamba na kuhakikisha anapata makazi bora ya kuishi
katika eneo lake jipya la Kazi”.
Sitaelewa
Halmashauri ambayo itashindwa kuzingatia maagizo haya kwa namna yeyeote
ile na ntaendelea kufuatilia mazingira ya mapokezi ya watumishi hawa,
sitaki mtumishi yeyote ashindwe kufanya kazi yake kwa ufanisi kwa sababu
ya mazingira magumu anayokutana nayo wakati wa kuripoti kazini,
Aliongeza.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi. Eliachi Macha
alisema Halmashauri imeandaa mazingira mazuri kwa ajili ya mapokezi ya
walimu wapya na pia watahakikisha wanatekeleza Maagizo yote ili
watumishi wote waweza kufanya kazi za ujenzi wa Taifa na kuleta matokeo
chanya.
Naye
Diwani wa Kata ya Mtera Mhe. Amon Kodi ambaye alishiriki katika ziara
hii alimpongeza Waziri Simbachawene kwa kazi kubwa anayoendelea kufanya
katika Kata yao, Jimbo la Kibakwe na Taifa kwa Ujumla na kumshkuru kwa
kufanikisha utekelezaji wa Miradi ya ujenzi wa bweni la Mtera Sekondari,
ukarabati wa zahanati ya kisima pamoja na ukarabati wa matundu ya vyoo
vya Shule vya Msingi Msangambuya.
Mhe.
Simbachawene yupo katika ziara ya Kikazi Wilayani Mpwapwa, Jimbo la
Kibakwe na ametembelea Kijiji cha Msangambuya, Chamsisili pamoja na
Chinoje.
0 comments:
Post a Comment