Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde,akizungumza na wafanyakazi wa Hospital ya Mkoa wa Dodoma.
Mbunge
wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde,akizungumza na wafanyakazi wa Hospital
ya Mkoa wa Dodoma hii leo,wakati wa uzinduzi mfumo wa Biometrics na
kamera za CCTV katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.
Mbunge
wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde,akibonyeza kitufe wakati wa kuzindua
matumizi ya mfumo wa Biometrics na kamera za CCTV katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Mbunge
wa Dodoma mjini Anthony Mavunde ameendelea kutatua kero katika sekta ya
Afya jimboni humo ambapo amezindua matumizi ya mfumo wa Biometrics
na kamera za CCTV katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,kufuatia
hali hiyo wagonjwa wengi waliokuwepo hospital hapo walionekana wenye
furaha na kuunga mkono jitihada za mbunge wao katika kusaidia kuboresha
huduma za Afya katika hospital hiyo.
Akizungumza
katika uzinduzi wa matumizi ya vifaa hivyo, Mavunde amesema ufungaji wa
mifumo hiyo ni miongoni mwa jitihada zake za kuhakikisha huduma za afya
katika jimbo hilo zinatolewa ipasavyo.
Mavunde
ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana
amesema mfumo huo umefungwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma na amelazimika
kufunga vifaa hivyo kutokana na malalamiko ya muda mrefu ya wagonjwa
kuwa wamekuwa wakitolewa lugha chafu na wauguzi.
Amesema
pamoja na kamera hizo, pia umefungwa mfumo wa Biometrics(uchukuaji
alama za dole gumba) ili kudhibiti watumishi ambao wamekuwa wakiondoka
kabla ya muda na kuchelewa kuingia kazini.
“Kamera
hizi zinarekodi sauti na kuchukua video ili kuondokana na malalamiko
yaliyotolewa na wananchi na itakuwa ni rahisi kumbaini mtu
atakayelalamikiwa na mgonjwa,”amesema Mavunde
Mavunde
amesema fedha alizotumia kununulia Kamera hizo na mfumo wa Biometrics
amezipata kwa kujibana katika mshahara wake lengo likiwa ni kutekeleza
ahadi yake aliyowaahidi wananchi wakati wa Kampeni kutatua kero za afya.
Aidha
amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza kasi ya utoaji huduma kwa
wananchi hasa ukizingatia kwasasa Dodoma kuna ongezeko la watu kutokana
na serikali kuhamia mkoani humo.
“Baadaye
pia tutaweka mfumo wa kuhifadhi mafaili, hii yote ni kurahisisha
utendaji kazi katika hospitali hii ili wananchi wetu waweze kupata
huduma za afya ipasavyo.pia nimeomba vifaa mbalimbali vya kisasa
Ujerumani kwa ajili ya hospitali hii tukipatiwa itasaidia sana utoaji
huduma za afya,”amesisitiza Mavunde
Amesema
ameahidi kutatua changamoto katika sekta ya afya ambapo mbali na
ufungaji vifaa hivyo alishakabidhi vitanda katika Zahanati na Vituo vya
afya 35
“Nimetoa
madawa kwenye kituo cha afya cha Makole yenye thamani ya Sh. Milioni
15,nimefunga umeme wa jua katika vituo vya Afya 17 pamoja na huduma za
macho kwa watu 7000 na watu 3000 walipata huduma za upasuaji
bure,”amesema
Naye,
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Caroline Damiani amemshukuru
Mbunge huyo huku akidai kuwa matunda ya ufungaji wa kamera yameanza
kuonekana kwa watumishi kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu
tofauti na awali.
“Kumekuwa
na kero nyingi kutoka kwa wagonjwa sasa Kamera za CCTV zitatusaidia
kutatua kero hizi na kudhibiti wale wanaotoka kabla ya muda wa kazi
kuisha au kuchelewa kazini,”amesema Mganga huyo
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Entersoft
Limited,Keneth Yindi amesema wamefunga Kamera 4 pamoja na mfumo wa
Biometrics katika hospitali hiyo na ina uwezo wa kurekodi matukio kwa
miezi tisa mfululizo.
0 comments:
Post a Comment