Imeandikwa na Anastazia Anyimike, Dodoma
SERIKALI imepokea Sh bilioni tisa kama gawiwo kutoka kwenye kampuni mbili ambazo serikali ina hisa.
Aidha, serikali imekubali kulifanyia kazi ombi la Kampuni ya Mafuta
ya Puma Energy la kutaka taasisi za umma, ziwe zinanunua mafuta ya
kampuni hiyo yenye ubia wa asilimia 50 kwa 50 na serikali ili faida
inayopatikana itumike kwenye kutatua changamoto za Watanzania.
Kampuni ya Mafuta ya Puma Renergy imetoa gawiwo la Sh bilioni saba
wakati Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta ya Tanzania (TIPER) imetoa gawiwo la
Sh bilioni mbili. Akijibu ombi lililotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya
Kampuni ya Puma, Dk Ben Moshi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip
Mpango (pichani) wakati akipokea gawio la Sh bilioni saba kwa serikali
ambayo ni faida iliyopatikana kutokana na biashara ya mafuta, alisema
watalifanyia kazi hasa kwa kutambua mchango wa kampuni zilizowekeza
nchini na zina ubia na serikali, na kutoa angalizo kuwa pamoja na ombi
hilo kufanyiwa kazi, hakuna sababu ya Puma kubweteka kwani lazima
ushindani uwepo ili kupatikana bidhaa bora.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment