Imeandikwa na Magnus Mahenge, Dodoma.
WANANCHI waliopimiwa viwanja mjini Dodoma na kupewa hati ya kumiliki
viwanja na maeneo hayo kwa miaka 33, wanabadilishiwa hati hizo na kupewa
za kumiliki miaka 99.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
akizungumza na vyombo vya habari mjini Dodoma juzi, alisema ubadilishaji
wa hati za kumiliki viwanja na maeneo hayo kwa miaka 99 unatolewa bure
bila kutozwa gharama zozote na utaanza Julai 10, mwaka huu ambako orodha
ya wananchi watakaonza kupata itatolewa.
Lukuvi alisema wizara itatoa orodha ya wananchi wa kwanza wa kupata
hati hizo mpya na wananchi hao watapitia manispaa ili kuhakiki nyaraka
zao na ndipo watafika kwa kamishna wa ardhi ili kupewa hati hizo mpya.
“Wananchi kabla ya kwenda wizarani kwenye kwenye ofisi za Kanda mjini
Dodoma, inatakiwa kupitia manispaa na kuhakiki taarifa zao na kama
wanadaiwa walipe madeni yao hadi mwaka huu 2017/18,” alisema Lukuvi.
Katika kuhakikisha ubadilishaji hati huo unakamilika, Lukuvi alisema
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imehamisha wakurugenzi
wanaohusika na masuala ya ardhi na kuimarisha Kanda ya Kati inayohudumia
mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro ili kutoa huduma kikamilifu
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment