Imeandikwa na Anastazia Anyimike, Dodoma
SERIKALI imesema mikataba iliyopo ya madini ni ya mwisho na kuanzia
sasa wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta hiyo watatumia leseni.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mjadala wa Muswada wa Sheria ya
Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali ya Mwaka 2017, Waziri wa Sheria na
Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi alisema sheria hii mpya ikisainiwa
itabadilisha mfumo huo kutoka kwenye mikataba na kuwa mfumo wa leseni.
“Tutafanya marejeo ya mikataba iliyopo, itatolewa taarifa ya mapitio
hayo kwa Bunge, sasa ungeendelea na mikataba ina maana tungekuwa
tumevunja hiyo mikataba. Sisi tunasema njooni kwa majadiliano, na niseme
hii ndio mikataba ya mwisho sheria hii ikipita hakuna tena mikataba na
hakuna leseni, hakuna mwekezaji ambaye atakuja baada ya sheria hii...
“Hiki kiporo cha mikataba baada ya hapo tunakwenda kwenye leseni.
Ndio maana hao hawataweza kutuburuza kwenye mahakama za usuluhishi kwa
sababu mikataba yao hatujaivunja, ila tumesema njooni tuzungumze. Lakini
tuzungumze nini? Hapo tunaangalia mambo ambayo hayakubaliki,” alieleza
Profesa Kabudi
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment