Imeandikwa na Sifa Lubasi, Dodoma.
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Saed Kubenea amefi kishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma
Mjini kujibu shtaka la kumshambulia mbunge mwenzake wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Juliana Shonza.
Kubenea alifikishwa mahakamani hapo jana mchana, na anatetewa na
mawakili watano. Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya,
James Karayemaha, Wakili wa Serikali Beatrice Nsana alidai mshtakiwa
alitenda kosa hilo Julai 3, mwaka huu kwenye Viwanja vya Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.
Wakili huyo alidai Kubenea alifanya kosa hilo ikiwa ni kinyume na
kifungu cha sheria namba 240 cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 16
kama ilivyofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.
Kubenea alikana shtaka hilo, na Hakimu Karayemaha alisema dhamana ya
mshtakiwa iko wazi na masharti ya dhamana ni kuwa na mdhamini mmoja
atakayesaini dhamana ya Sh milioni moja na mdhamini atatakiwa kuwa na
barua ya Mtendaji wa Kijiji au Kata.
Alikamilisha masharti ya dhamana na kudhaminiwa. Juzi, wabunge saba
wa Chadema walikamatwa na Polisi mkoani hapa na kuhojiwa kwa siku mbili
kuhusu shambulio dhidi ya Shonza ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu.
Hao ni Suzan Kiwanga (Mlimba), Kubenea (Ubungo), Cecilia Pareso (Viti
Maalumu), Frank Mwakajoka (Tunduma), Joseph Selasini (Rombo) na Pauline
Gekul (Babati Mjini).
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment