Imeandikwa na Anastazia Anyimike, Dodoma
BUNGE limeagiza Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), kuitwa mbele
ya Kamati ya Kudumu ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kuhojiwa
kutokana na utovu wa nidhamu kwa kauli za kumdhalilisha spika.
Agizo la Spika limetolewa ikiwa ni siku moja tangu Mdee awekwe ndani
kwa saa 48 na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Ally
Salum Hapi kwa kutoa kauli ya kumdhalilisha Rais John Magufuli.
Mdee na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya pia wa Chadema wanatumikia
adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza kabla ya kuahirisha shughuli za
Bunge juzi jioni, alisema Halima amekuwa akimdhalilisha Spika katika
mitandao ya kijamii.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment