Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.
Serikali
kupitia Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo imesema kuwa
inakamilisha mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Michezo ya mwaka 1995 ili
kuhakikisha inaendana na mahitaji ya sasa katika maendeleo ya michezo
nchini.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Anastazia Wambura wakati akijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini
Mhe.Cosato Chumi aliyetaka kujua mipango ya Serikali katika kufufua
mchezo wa Riadha Bungeni Mjini Dodoma leo.
“Serikali
kwa kushirikiana na wadau inatekeleza programu mbalimbali za kuendeleza
mchezo wa riadha nchini ikiwemo Kilimanjaro Marathon,Bagamoyo
Marathon,Heart Marathon na Tulia Marathon ambayo hushirikisha wanariadha
kutoka nje”,Aliongeza Mhe.Wambura.
Aidha
pamoja na hayo Mhe.Wambura amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI
imeendesha mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA ambayo pamoja na mambo
mengine yanalenga kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wetu katika
mchezo wa riadha.
Akizungumzia
suala la miongozo ya Kiserikali amesema kuwa Wizara yake inakamilisha
taratibu za kuandaa miongozo ya kiserikali ili kuwezesha wadau wote
kuendesha shughuli zao katika mazingira ya weledi na stadi bora za
michezo.
Hata
hivyo Naibu Waziri uyo amesema kuwa nchi yetu imeanza kufanya vizuri
katika mashindano ya Riadha kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma
kupitia kwa wanariadha wake kama Francis Naal,Samson Ramadhani,Gidamis
Shahanga,Juma Ikangaa,Suleiman Nyambui na Filbert bayi na hivyo
kuitangaza nchi yetu.
“Nchi
yetu kwa sasa imeanza kupata mafanikio katika riadha kupitia wanariadha
wetu kama Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya dhahabu kwenye
mashindano ya standard Chartered Mumbai Marathon,Cecilia Ginoka Panga
aliyeshinda Beijing International Half Marathon na Giniki Gisamoda
aliyeshinda Shanghai International Half Marathon,wote hawa wanaitangaza
nchi yetu vizuri na kuifanya ifahamike na hivyo kuvutia watalii
”Alisisitiza Mhe.Wambura.
0 comments:
Post a Comment