Na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.
Serikali
kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema imeandaa mtaala
mpya ambao umeandaliwa katika misingi ya elimu jumuishi ambao ulianza
kutumika kuanzia mwaka wa masomo 2014/2015 ili kumudu wanafunzi wenye
mahitaji maalum.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Eng,Stella
Manyanya wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Stella Ikupa
Alex aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kila
mwalimu anapatiwa mafunzo maalum yatakayomwezesha kufundisha wanafunzi
wenye ulemavu.
“Hadi
sasa wahitimu wa ngazi ya Stashahada ya Elimu maalum wapatao 158
wamehitimu Octoba 2016 na wanachuo 248 wanaendelea na masomo katika chuo
cha Ualimu Patandi”,Aliongeza Mhe.Manyanya.
Aidha
Waziri uyo amesema kuwa kutokana na umuhimu wa walimu hawa Wizara yake
katika mwaka wa fedha 2016/17 iliendesha Mafunzo kwa walimu 519 walio
kazini wanaofundisha darasa la kwanza na la pili kuhusiana na mtaala
ulioboreshwa ili kumudu ufundishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Pamoja
na hayo tarehe 20 mpaka 28 Juni,2017 walimu 712 walio kazini
wanaofundisha wanafunzi wenye ulemavu wa akili na wenye usonjo
walipatiwa mafunzo katika vituo vya Mwanza,Arusha,Mbeya na Morogoro ili
kuwajengea uwezo wa kumudu ufundishaji wa wanafunzi wenye ulemavu huo.
0 comments:
Post a Comment