Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Muonekano
wa sehemu ya juu ya daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205
linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga (wapili kushoto), akiwa na wataalamu wanaosimamia
ujenzi wa barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), inayojengwa kwa
kiwango cha lami mara baada ya kuikagua mkoani Dodoma. Wanne kushoto ni
Mkurugenzi wa barabara Eng. Ven Ndyamukama.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.
Joseph Nyamhanga, akikagua sehemu ya barabara ya Mela – Bonga (km 88.8),
inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Manyara.
Ujenzi wa barabara ya Dodoma – Babati kwa kiwango cha lami sehemu ya Mela – Bonga (km 88.8), ukiendelea.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS), mkoa wa Manyara, Eng. Bashiri Rwesingisa (kulia), na
mkandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group Co. Ltd anayejenga
sehemu ya Mela – Bonga (km 88.8), mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa kampuni ya
CHICO anayejenga sehemu ya barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35),
alipofanya ukaguzi mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga, akikagua kingo za daraja la Kelema lenye urefu wa
mita 205 linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga, amewaagiza Mameneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS), mkoa wa Dodoma na Manyara kuhakikisha wanatafuta eneo la
kujenga kituo cha mizani ili kudhibiti madereva wanaozidisha uzito
katika barabara ya Dodoma- Babati (km 263), inayojengwa kwa kiwango cha
lami.
Akizungumza
katika eneo la Bonga, mkoani Manyara Eng. Nyamhanga, amesema kuwa
barabara hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika baadae mwezi huu inahitaji
uwepo wa mizani kwa haraka ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito na
kuharibu barabara.
"Hakikisheni
mnatafuta eneo la kujenga mizani ndani ya miezi miwilli ambapo
wakandarasi bado wapo hapa ili iwe rahisi kwenu kumtumia mmoja wa
wakandarasi hawa kuweza kujenga kituo hiki haraka, uwepo wa mizani hii
utasaidia kudhibiti magari makubwa yanayozidisha uzito", amesema Katibu
Mkuu Nyamhanga.
Aidha,
Eng. Nyamhanga amewaagiza mameneja wote nchini kuchukua hatua kali za
kisheria kwa watu wote wanaopitisha mifugo katika barabara ili kudhibiti
uharibifu wa barabara.
Amewataka
madereva wote nchini kuendesha magari yao kwa tahadhari na kuzingatia
alama za barabarani ili kudhibiti ajali zinazoepukika.
Katibu
Mkuu Nyamhanga ametoa wito kwa wananchi wanaoishi kando ya barabara
hiyo kuhakikisha wanatumia fursa ya kukamilika kwa barabara hiyo kwa
ajili ya kuleta maendeleo katika maeneo yao ili kukuza uchumi kwa
familia zao na Taifa kwa ujumla.
Amemataka
mkandarasi wa sehemu ya barabara ya Mela - Bonga (km88.8) kuhakikisha
anakamilisha kazi zilizobaki kwa wakati na kwa viwango vilivyo kwenye
mkataba.
Katika
hatua nyingine, Eng.Nyamhanga, ametembelea na kukagua barabara ya
Mayamaya- Mela (km 99.35) kwa kiwango cha lami na daraja la Kelema lenye
urefu wa mita 205 na kuridhishwa na ujenzi wake na kumtaka mkandarasi
wa mradi huo kukabidhi mradi huo ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.
Kwa
upande wake, Mhandisi Mshauri wa barabara ya Mayamaya- Mela (km 99.35),
Leornado Licari, amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kumaliza mradi huo
kwa wakati kwani kazi zilizobaki kwa sasa ni ndogo kama kumaliza tabaka
la mwisho la lami na uwekaji wa alama za barabarani.
Barabara
ya Dodoma- Babati (km 263) ni sehemu ya barabara kuu ya kaskazini
(Great North road), inayoanzia Capetown nchini Afrika Kusini hadi Cairo
nchini Misri ambapo hapa nchini barabara hiyo inayopitia Tunduma mkoani
Mbeya, hadi Namanga mkoani Arusha ina urefu wa kilomita 1500,hivyo
kukamilika kwa sehemu ya barabara ya Dodoma – Babati (km 263),
kunaiunganisha barabara yote kutoka Capetown hadi Cairo yenye urefu wa
kilomita 100000 kwa kiwango cha lami.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
0 comments:
Post a Comment