Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Spika
Mstaafu Anna Makinda akikaribishwa na Mkuu wa Masoko wa benki ya
kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame katika banda lao katika Maonesho ya Nane
nane yanaoendelea Mkoa wa Dodoma.
Spika Mstaafu Anna Makinda akisoma moja ya kipeperushi cha benki ya DCB katika banda lao katika Maonesho ya Nane nane yanaoendelea Mkoa wa Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Masoko wa benki ya kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame
Wananchi wakipatiwa huduma katika banda la benki ya DCB katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mkoani Dodoma.
Spika
Mstaafu Anna Makinda ameipongeza DCB Commercial Bank kwa huduma bora za
kibenki inayotoa hasa huduma za mikopo kwa wajasirimali wadogo wadogo
na kuwakwamua katika hali ya umasikini.
Makinda
amewaasa DCB Commercial Bank kujikita zaidi kutoa huduma hii kwa
wajasiriamali wadogo wadogo vijijini ambao ndiyo wengi nchini ili
kuboresha hali za maisha yao kwa kuwapatia mikopo.
Hayo
aliyasema wakati alipotembelea banda la DCB Commercial bank katika
maonesho ya nane nane kanda ya kati yanayoendelea mkoani Dodoma. Makinda
aliongezea kuwa ili kuwezesha wajasiriamali wengi DCB Benki haina budi
kupeleka huduma hii ya mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo wadogo
vijijini ambako kuna uhitaji mkubwa wa huduma hii ya mikopo ya vikundi
Sambamba na utoaji wa mikopo hii ya vikundi kwa wajasiriamali wadogo
wadogo.
Makinda
ameasa DCB kuwaunganisha wajasiriamali hawa na huduma ya bima ya afya
kutoka NHIF na pia bima ya taifa ya Jamii ili wateja hawa au familia zao
wanapougua wapate msaada wa matibabu kwa unafuu hivyo kuwafanya wawe na
afya na kuweza kurejesha mikopo .
Alisisituza
kuwa mteja akiugua ile pesa ya marejesho ataitumia katika kugharamia
matibabu hivyo kuitia hasara benki, kumbe akijiunga na mifuko ya afya ya
jamii atapata matibabu bure hivyo benki haitaathirika. Alisema makinda.
Akimkaribisha
kwenye banda na kuelezea huduma zinazotolewa na DCB Commecral Bank,
Meneja masoko wa DCB benki Boyd Mwaisame alitaja huduma za DCB
zinazopatikana katika banda la benki hiyo viwanja vya maonesho nane nane
Mzuguni Dodoma kuwa ni pamoja na kufungua akaunti za kuweka akiba kwa
watu binafsi, akaunti za wanafunzi, akaunti za muda maalumu, akaunti za
biashara na huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo, wakati na
wakubwa.
Mteja
akisha fungua akaunti ya akiba na biashara anunganishwa bure na huduma
ya DCB Pesa, huduma mpya ya kufanya miamala ya benki kupitia simu ya
mkononi, yaani kuweka na kutoa pesa na kulipia bili mbalimbali. Huduma
hii si lazima mteja awe na akunti DCB, bali mtu yeyote mtaani anaweza
kujiunga mradi tu awe na namba yoyote ya simu ya mkononi iliyosajiliwa
na mojawapo ya kitambulisha cha mpiga kura, utaifa, udereva na paspoti.
Huduma
hii inapatikana kwa kupiga *150*85#. Pia Meneja masoko alimueleza Mh.
Makinda kuwa huduma za DCB Commercial Bank mbali na Dar es Salaam kwa
sasa pia zinapatikana mkoani Dodoma kupitia tawi lake lilifunguliwa
hivi karibuni katika jengo la LAPF mtaa wa Makole na mikoa mbali mbali
kupitia huduma ya uwakala wa benki yaani DCB Jirani.
Naye
afisa wa benki Cecilia Msikula akimuelezea Mh. Makinda huduma ya akiba
ya watoto akaunti za watoto –Young saver account ambayo alivutiwa sana
nayo hasa Meli ya mtoto, alisema kuwa DCB inatoa huduma hii bila makato
ya mwezi ambapo mteja akisha fungua akaunti ya mtoto kwa shi. 5,000 tu
anapewa Meli ya Mtoto/ kibubu bure kumjengea mtoto utamaduni wa
kujiwekea akiba akiwa bado mdogo kwa ajili ya matumizi yake ya baadaye.
Pesa ikisha jaa kwenye Meli ya mtoto yaani kibubu mzazi analeta benki
kwa ajili ya kuziweka kwenye akaunti ya mtoto baada ya kuzihesabu.
Katika
msafara huo, Spika mstaafu Makinda aliongozana na viongozi mbalimbali
akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mpwawa Mh. Jabir Shekimweri.
0 comments:
Post a Comment