Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa DK. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Mkutano Mkuu wa Skauti wa Dunia mjini Baku, Azerbaijan
Rais
Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa DK. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 100 ya Skauti nchini
zilipofanyika mkoani Dodoma mwezi Julai. Pamoja naye ni Skauti Mkuu
Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza (kushoto). Kamishna Mkuu Mheshimiwa
Abdulkarim Esmail Shah (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan
Rugimbana
Rais
Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa DK. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa Mkutano Mkuu wa Skauti wa Dunia huko Baku nchini Azerbaijan
Mkutano Mkuu wa Skauti wa Dunia unafanyika nchini Azerbaijan katika
mji wa Baku kuanzia tarehe 14 hadi 18 Agosti 2017. Mkutano huu utajumuisha nchi
zote wanachama ambao zinafikia nchi 167. Kila nchi inapaswa kutuma wajumbe 6
kuhudhuria mkutano huu, lakini pia waangalizi (Observers) wanakaribishwa.
Ni mkutano mkuu ambao unazungumzia masuala mbalimbali yanayohusu
mafunzo kwa vijana skauti, miradi mbalimbali, mafanikio na changamoto
mbalimbali zinazokabili nchi wanachama.
Tanzania inawakilishwa na wajumbe 6 muhimu kama Katiba ya Shirikisho
la Vyama vya Skauti Duniani (World Scout Bureau) inavyosema, lakini pia ujumbe
huo unaongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa DK. Jakaya Mrisho
Kikwete, kama Mlezi Mstaafu wa Chama cha Skauti Tanzania. Kwa kawaida Mlezi wa
Chama cha Skauti Tanzania ni Rais wa Nchi kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha
Skauti Tanzania.
Mheshimiwa DK. Jakaya Kikwete amepewa Heshima ya kuwa Msemaji Mkuu (Keynote
Speaker) wa ujumbe wa Chama cha Skauti Tanzania.
Ujumbe wa Chama cha Skauti Tanzania tayari umeshaondoka nchini
kuhudhuria Mkutano huo, ambapo Mheshimiwa DK. Jakaya Kikwete ameomba kukutana
na Viongozi wa Vyama vya Skauti nchi za Afrika kuzungumza na kujadiliana
masuala mbalimbali yanayohusu uskauti barani Afrika wakati wa Mkutano Mkuu huo.
Ujumbe wa Chama cha Skauti Tanzania ni pamoja na Skauti Mkuu
Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza. Kamishna Mkuu Mheshimiwa Abdulkarim Esmail
Shah. Naibu Kamishna Mkuu ndugu Rashid Kassim Mchatta. Kamishna Mtendaji Bi.
Eline Kitaly. Na Kiongozi wa skauti kutoka mkoa wa Dar es salaam ndugu. Dinesh
Rajah.
Chama cha Skauti Tanzania kimetimiza Miaka 100 tangu kuanzishwa kwake
hapa nchini, na sherehe za maadhimisho hayo zilifanyika mkoani Dodoma kuanzia
tarehe 21 hadi 28 Julai 2017 ambapo Viongozi mbalimbali wa Kitaifa walialikwa
wakiwemo Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu, pamoja na Skauti wenyewe kutoka ndani
na nje ya Nchi.
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa
Maadhimisho hayo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan ambaye alimuwakilisha Rais DK.
John Pombe Magufuli.
Tuzo na Nishani kadhaa zilitolewa kwa Viongozi mbalimbali wa Nchi,
Viongozi wa Skauti, na skauti wenyewe ambao wameshiriki katika matukio ya
ujasiri, michezo na mashindano za stadi za kiskauti.
Maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania yalifungwa na Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi.
Ujumbe wa Viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania ambao wanahudhuria
Mkutano Mkuu wa Skauti wa Dunia pia
utapokea Tuzo na Cheti maalum cha
kutimiza Miaka 100 ya uskauti Tanzania, ujumbe huo unatarajia kurejea nchini tarehe 21 Agosti
2017.
IMETOLEWA NA HIDAN
.O. RICCO.
KAMISHNA
MKUU MSAIDIZI
0 comments:
Post a Comment