Home » » VIONGOZI WAPYA UVCCM WILAYA YA CHAMWINO WAFANYIWA SEMINA KUWAJENGEA UWEZO

VIONGOZI WAPYA UVCCM WILAYA YA CHAMWINO WAFANYIWA SEMINA KUWAJENGEA UWEZO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

  Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma Asia Abdulkarim Halamga akimkabidhi mmoja wa viongozi wa matawi kadi za UVCCM
 Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma Asia Abdulkarim Halamga ameongea na viongozi wa Mashina, Matawi na Kata huko Buigiri Wilayani Chamwino ikiwa ni sehemu ya semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni waweze kutambua majukumu yao, wafanye kazi bila kuingiliana kwa maslahi ya Chama na serikali.

Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma Asia Abdulkarim Halamga ameongea na viongozi wa Mashina, Matawi na Kata huko Buigiri Wilayani Chamwino ikiwa ni sehemu ya semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni waweze kutambua majukumu yao, wafanye kazi bila kuingiliana kwa maslahi ya Chama na serikali.

Ameyasema hayo ikiwa ni mpango maalum wa vijana wa Chama cha Mapinduzi kuwapiga msasa viongozi wake ili waweze kuisimamia serikali katika kutekeleza majukumu yake.

Asia Halamga amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa juhudi na uadilifu mkubwa ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali kwa ujumla lakini pia kubuni miradi itakayowawezesha kujitegemea kiuchumi kwani wao ndiyo taswira ya Chama hivyo wanapaswa kuwa mfano bora kwa jamii.

Sambamba na mafunzo hayo pia ametoa kadi 252 za umoja wa vijana UVCCM pamoja na kanuni katika matawi ya Makulu, Buigiri, Mwegamile na Chinangali II ambapo kila tawi limepata kadi 63 kwa lengo la kuongeza wanachama wa UVCCM na sehemu ya malipo yake itumike kutunisha mifuko ya matawi yao.

Naye Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Kenneth Yindi aliahidi kufanyia kazi Agizo la Katibu wa UVCCM mkoa wa Dodoma la kutatua changamoto ya kutokuwepo kwa ofisi ya Kata kwa kujenga ofisi, Ambapo ujenzi huo unaanza kufanyika mwezi tisa mwaka huu kwa kushirikiana uongozi wa umoja wa vijana na wanachama wake katika Kata ya Buigiri, ambapo Katibu wa UVCCM Mkoa aliahidi mara watakapokuwa tayari atawaunga mkono katika ujenzi wa Ofisi hiyo. 

Pia Diwani alipokea Agizo la kuzitafutia mashamba Jumuiya tatu za Vijana, Wazazi na Wanawake watakayoyatumia kujiingizia kipato ili waweze kujitegea kiuchumi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa