Home » » WIZARA YA ARDHI YATAMBULISHWA NA KOREA MRADI WA KUCHORA RAMANI ZA KIJIOGRAFIA

WIZARA YA ARDHI YATAMBULISHWA NA KOREA MRADI WA KUCHORA RAMANI ZA KIJIOGRAFIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Timu ya utambulisho wa Mradi wa kuchora Ramani za kijiografia kutoka Korea na baadhi ya watendaji wa Idara ya Upimaji wa Ramanni (Wizara ya Ardhi) katika Mkutano wa utambulisho wa Mradi. 
Ugeni kutoka Taasisi ya Taifa ya Kijiografia- Korea, waliofika kutambulisha Mradi wa kuchora Ramani za kijiografia utakaoanza 2018, katika picha ya pamoja na baadhi ya watenfaji wa Wizara ya Ardhi.

Ugeni wa Wakorea, kutoka Taasisi ya Taifa ya masuala ya kijiografia umetambulisha rasmi mradi wa kuchora ramani za kijiografia kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Ugeni huo uliopokelewa na Idara ya Upimaji na Ramani katika Wizara ya Ardhi, umehusisha timu ya Maafisa kumi kutoka nchini Korea. Akizungumza na wawakilishi wa Idara ya Upimaji na Ramani; Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Taasisi hiyo; Bwn. Hynu-Hee Joo amesema mradi huo unaojumuisha nchi tatu, yaani Tanzania, Zambia na Msumbiji unategemewa kuanza rasmi 2018.

Mradi wa kuchora ramani za kijiografia upo chini ya ufadhili wa nci ya Korea kupitia Benki ya Dunia na Umoja wa Kamisheni ya Afrika.

Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa