Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Suleiman
Jaffo akiongea na wajumbe wa Mkutano wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kutoka
Tanzania na Afrika Kusini walipokuwa ziarani Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Wa
kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi na kulia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano Serikalini
Bi. Plumla Williams akitoa neno kwa niaba ya wajumbe kutoka Afrika Kusini
walipotembelea maeneo ya ukombozi yaliyopo Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ikiwa
ni sehemu ya agenda ya Mkutano kuhusu utekelezaji wa Programu ya Urithi wa
Ukombozi wa Bara la Afrika.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Suleiman
Jaffo (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkurungenzi Mkuu wa Kazi za Umma kutoka
Afrika Kusini Bw. Mziwonke Dlabantu (kulia). Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi.
Baadhi ya Viongozi
kutoka Afrika Kusini wakiangalia makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini yaliopo
Wilayani Kongwa, Dodoma. Picha na Eleuteri
Mangi, WHUSM, Dodoma.
Na Bearice
Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Naibu Waziri Ofisi ya
Rais-TAMISEMI Suleiman Jaffo amesema kuwa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa
Bara la Afrika (ALHP) una historia adhimu kati ya Tanzania na Afrika Kusini na itasaidia
kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Mhe.
Jaffo ameyasema hayo
leo Wilayani Kongwa, Dodoma wakati wa ziara ya Makatibu Wakuu,
Wakurugenzi na
Watalamu wa Programu hiyo kutoka Tanzania na Afrika Kusini kujionea
maeneo yaliyotumika wakati wa Ukombozi wa Bara la Afrika ikiwemo Afrika
Kusini.
“Nchi ya Tanzania na
Afrika Kusini zina urafiki mkubwa na wa karibu kuliko nchi nyingine yeyote Afrika,
hivyo kupitia Programu hii tutazidi kuimarisha udugu na uhusiano uliopo”
amefafanua Mhe. Jaffo.
Ziara hiyo ilihusisha
maeneo ya makaburi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini, Kambi walipokuwa
wanaishi, mahandaki walipokuwa wanajihifadhi dhidi ya maadui pamoja na madarasa
yaliyotumika kwa ajili ya mafunzo kwa wapigania uhuru.
0 comments:
Post a Comment