Home » » JAFO AWAONYA WAKANDARASI WASHAURI WA MIRADI YA MAJI

JAFO AWAONYA WAKANDARASI WASHAURI WA MIRADI YA MAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Naibu Waziri Ofisi ya Rasi, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa wataalam wa maji.
Naibu Waziri Ofisi ya Rasi, Tamisemi Selemani Jafo akisikiliza taarifa ya mradi wa maji Mkoyo.
Baadhi ya wajumbe wa kijiji cha Mkoyo pamoja na wataalam wa maji wa manispaa ya Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo.
jenerata ya mradi wa maji Mkoyo.

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amesikitishwa na baadhi ya wakandarasi washauri wanaosimamia miradi ya maji katika halmashauri mbalimbali hapa nchini kwa kutofanya kazi yao kwa umakini na hivyo kuruhusu wakandarasi wa ujenzi wa miradi ya maji kujenga miradi hiyo chini ya kiwango.

Jafo alitoa kauli hiyo alipotembelea mradi wa maji katika kijiji cha Mkoyo ndani ya Manispaa ya Dodoma, ambapo amebaini mkandarasi mshauri wa mradi huo O&A Co LTD hakuwa makini wakati wa utekelezaji wa mradi huo kwani imeonekana mradi huo ukiwa na changamoto kadhaa licha fedha nyingi kutumika zaidi ya milioni 430 kati ya milioni 480 zilizipangwa kwa mradi huo.

Amesema wakandarasi hao wamekuwa wakisababisha miradi kujengwa chini ya kiwango na kusababisha kushindwa kuwapatia maji wananchi kama ilivyotarajiwa. Aidha amebaini kampuni hiyo mshauri huyo ndiye yule yule aliyesimamia mradi kijiji cha Itiso ambao

aliutembelea mradi huo mwezi Agosti mwaka huu na kukumbana na changamoto nyingi.Kufuatia hali hiyo, Jafo amemuagiza Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Rais Tamisemi Mhandisi Enock kwa shirikiana na wahandisi wa maji wa halmashauri za mkoa wa Dodoma kufanya tathmini ya miradi yote ya maji inayosimamiwa na mshauri huyo ili Ofisi ya Tamisemi ifanye maamuzi sahihi.

Aidha amesema serikali haitaweza kuvumilia endapo ikibainika mshauri wa miradi hiyo ameshindwa kuisaidia serikali katika miradi ya maji anayoisimamia.

Naibu waziri Jafo amezitaka kampuni zote za washauri waelekezi kutimiza wajibu wao katika kusimamia miradi ya maji kwani wananchi wamekuwa wakitaabika sana kutokana na kero ya maji ilihali wao wamechukua dhamana ya kusimamia miradi hiyo ya serikali.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa