Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma
(PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga (kushoto) akiongea wakati
wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya
Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini
Dodoma, Kulia ni Mjumbe wa Bodi hiyo Prof. Sufian Bukurura.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA)
Balozi Dkt. Matern Lumbanga wakati wa makabidhiano ya Ripoti ya Tathmini
ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma
(PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga akimkabidhi Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa
Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akikata utembe baada ya kupokea
Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini
Dodoma, Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya
Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akionesha kwa wanahabari na
wajumbe wengine wa Bodi(hawapo pichani) kitabu cha Ripoti ya Tathmini ya
Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, , Kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wajumbe wa Bodi ya
ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) baada ya kupokea
Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini
Dodoma ambapo ameahidi kuzichukulia hatua taasisi zote zilizokiuka
taratibu za manunuzi zilizoainishwa kwenye Ripoti ya Tathmini ya
Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt. Laurent
Shirima akiongea, wakati wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha
2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na
wajumbe wa Bodi ya ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Serikali
imesema itazichukulia hatua Taasisi zote zilizokiuka sheria na kanuni
za manunuzi ya Umma pamoja na zile zenye viashiria vya rushwa ambazo
zimebainika katika ripoti ya tathmini ya utendaji iliyotolewa na Mamlaka
ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa mwaka wa Fedha 2016/17.
Hayo
yamesemwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip
Mpango alipokuwa akipokea ripoti ya tathimini ya utendaji wa Taasisi za
Serikali katika sekta ya Manunuzi iliyofanywa na PPRA kwa mwaka wa Fedha
2016/17.
“Tutazichukulia
hatua na kuziwajibisha taasisi zote ambazo zimebainika katika ripoti
hii kuwa na viashiria vya rushwa au kufanya malipo yenye utata katika
manunuzi yao,” alisema Dkt. Mpango.
Dkt.
Mpango amesema kuwa, zaidi ya 70% ya fedha za Umma zinatumika kununua
vifaa na huduma mbalimbali hivyo Serikali haitavumilia kuona fedha hizo
zinatumika bila kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.
Aidha,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA Balozi Dkt. Matern Lumbanga
amezitaja taasisi ambazo zimekiuka sheria na taratibu za manunuzi kwa
mwaka 2016/2017 kuwa ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Taasisi ya
Mifupa (MOI) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taasisi
nyingine ni Shirika la Bima la Taifa (NIC), Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), Mamlaka ya Anga (TCAA), Wizara ya Fedha na Mipango na
Halmashauri ya Wilaya Kondoa.
Balozi
Lumbanga amesema kuwa uchunguzi wa zabuni mbili zenye thamani ya
shilingi bilioni 160.5 ambazo zilikuwa zinatekelezwa na Wizara ya Fedha
na Mipango pamoja TCAA haukubainika mapungufu ya msingi na PPRA
ilipendekeza utekelezaji wa miradi hiyo uendelee kama ilivyopangwa.
“Uchunguzi
uliofanywa katika taasisi sita zilizobaki ulibaini kuwa Serikali
ilipata hasara ya takribani shilingi milioni 12.15 kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo, ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi
uliosababisha ongezeko la riba pamoja na faini zilizotokana na ukiukwaji
wa taratibu za kijamii na mazingira kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa
kazi za ujenzi,” alisema Balozi Lumbanga.
Balozi
Lumbanga amezitaja Taasisi zilizobainika na malipo yenye utata kuwa ni
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL) na Halmashauri ya Kwimba. Ukaguzi wa kupima upatikanaji wa
thamani ya fedha ulibaini malipo yenye utata katika taasisi hizo tatu
ambazo ni kiasi cha shilingi milioni 483.44 zililipwa kwa wakandarasi
kwa kazi ambazo hazikuwa zimefanyika.
Vile
vile amesema kuwa, miradi 33 katika taasisi 17 ilibainika kuwa na
kiwango kikubwa cha viashiria vya rushwa. Taasisi hizo ni Mamlaka za
Maji Safi na Maji Taka za Moshi (Muwasa), Mwanza (Mwauwasa) na Arusha
(Auwasa) pamoja na Halmashauri ya Wilaya za Wilaya za Msalala, Kibondo
na Moshi.
Taasisi
byingine ni Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Wizara
ya Maji na Umwagiliaji, Chuo cha Ufundi Arusha, Halmashauri ya Mjia wa
Kahama, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Uhasibu Arusha
(IAA), Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Halmashauri ya Mji wa MAsasi
pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Ripoti hiyo ni ripoti ya 11 kuwasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango tangu PPRA ilipoanzishwa
0 comments:
Post a Comment