Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selamani
Jafo akifungua kongamano ya Chama cha Wahasibu Tanzania linalohusu
uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa
linalofanyika Mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wahasibu Tanzania Fred Msemwa akitoa neno la utangulizi
wakati wa ufunguzi wa Kongamano linalohusu uwazi na uwajibikaji kwa
viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Washiriki
na wajumbe wa chama cha Wahasibu Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa kabla
ya Ufunguzi wa Kongamano lililofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa Mhe.Selemani Jafo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
Mhe.Selemani Jafo(kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu
Tanzania Fred Msemwa wakati wa Ufunguzi wa Kongamano linalofanyika
Mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
Mhe.Selemani Jafo(Katikati mbele) akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa chama cha wahasaibu Tanzania pamoja na wawwezeshaji wa
Kongamano hilo.
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani
Jafo amewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kudhibiti
matumizi yasiyo ya lazima kwenye Halmashauri ili kufanikisha utekelezaji
wa miradi ya maendeleo.
Waziri
Jafo ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa kongamano la siku mbili la
Chama cha Wahasibu Tanzania(TAA) lililojumuisha wataalam wa Hesabu na
wafanya maamuzi kutoka katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Katika
Kongamano hilo ambalo Linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa
kwa Chama hicho mwaka 1983 limelenga kujenga uwezo kuhusu Uwazi na
Uwajibikaji kwa Viongozi waandamizi wa Mamlaka ta Serikali za Mitaa
katika Matumizi ya Fedha za Umma.
Waziri
Jafo amesema kuwa Bajeti kubwa ya Serikali inapelekwa kwenye Mamlaka za
Serikali za Mitaa takribani asilimia 20.7 ya Bajeti ya Serikali
huelekezwa katoka Halmashauri hivyo ni eneo ambalo linapata Fedha
nyingi na zinahitajo uangalizi mkubwa.
Tunafahamu
kuwa Viongozi wa Halmashauri mna Mamlaka kamili ya kupanga matumizi ya
Fedha hizo lakini angalieni maeneo ambayo yataleta Tija kwa Wananchi na
yatatatua changamoto zinazowaathiri wananchi wetu katika maisha yao ya
kila siku, huko ndio sehemu ya kutumia Fedha nyingi na si vinginevyo.
Katika
maeneo ambayo hayanipi amani na bado nayaona kuwa na matumizi mabaya ya
Fedha ni eneo la Manunuzi ya Umma nawasihi muwaelimisha vya Kutosha
viongozi hawa namna ya kudhibiti mianya yote ya Upotevu wa Fedha uliopo
katika eneo la Manunuzi"
Alisema Jafo.
Aliongeza
kuwa kuna tabia ya kubadilisha matumizi ya vifungu"Realocation" bila
sababu za Msingi na bila kufuata taratibu zinazohitajika suala hili
limekua likisababisha hoja nyingi wakati wa Ukaguzi wa Hesabu nawasili
viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa mkaliangalie hilo kwa jicho la
tati na mkalidhibiti.
Akitoa
neno la Ufunguzi Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzani Fred Msemwa
amesema Chama hiki kina umri wa Miaka 34 na kina lengo la kuendeleza
Taaluma za Uhasibu Tanzania na kutoa elimu ya Fedha na Biashara kwa
wananchi ili waweze kujisimamia katika mapato na matumizi yao.
Msema
alisema kuwa wamefanikiwa kutoa elimu ya Kodi, Ongezeko la
Thamani,sheria za Fedha na mabadiliko yake pamoja na kuanzisha Dawati la
Mhasibu ambalo hutoa uelewa kwa wananchi kuhusu masuala ya Fedha,
biashara na Rasilimali.
Kongamano
hili ni endelevu na litakua likifanyika kila mwaka na litakuwa
likiwajengewa uwezo viongozi wa Serikali ambao wengine hawana utaalam wa
Uhasibu namna ya kuipitia kwa umakini taarifa ya Mkaguzi wa Ndani,
viashiria vya Rushwa katika matumizi ya Fedha za Umma, kuzuia
vihatarishi, namna ya kuongeza vyanzo vya mapato na namna ya kupata
Fedha za Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
0 comments:
Post a Comment