SERIKALI
imewalipa pensheni wafanyakazi 245 wa iliyokuwa Kampuni ya Simu ya
TTCL, chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kiasi cha shilingi bilioni
12.7.
Hayo
yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Ludewa Mhe.
Deogratias Ngalawa, aliyetaka kufahamu, lini Serikali ingewalipa
wafanyakazi wa TTCL wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki madai ya
pensheni yao.
Dkt.
Kijaji alisema kuwa malipo hayo yamefanyika kwa wafanyakazi 245 ambao
wamelipwa fedha zao kwa mkupuo ambapo kati yao wastaafu 54 walifariki
dunia na malipo yao kulipwa warithi wao.
“Wastaafu 198 wanaendelea kulipwa malipo ya nyongeza ya pensheni ya kila mwezi” alisema Dkt. Kijaji.Alisema
kuwa malipo hayo yanafuatia uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi namba
69/2005 ambapo wafanyakazi hao 254 waliishitaki Serikali kupinga uamuzi
wa kusitisha mfuko uliojulikana kama East Africa Non Contributory
Pension Scheme.
“Katika
Shauri hilo, Mahakama Kuu iliamua kuwa, uamuzi wa Serikali kusitisha
mfuko huo haukuwa sahihi kisheria na hivyo kuamua wafanyakazi 254
waliokuwa katika shauri hilo walipwe madai yao ambayo yalijumuisha
malipo ya mkupuo, riba pamoja na pensheni yao ya kila mwezi” aliongeza
Dkt. Kijaji.
Alisema
kuwa baada ya uamuzi huo wafanyakazi wengine 324 nao walifungua kesi
Makahama Kuu wakitaka walipwe pensheni kama wenzao walivyolipwa wakati
hawakuwa sehemu ya wafanyakazi waliofungua na kushinda kesi hapo awali.“Mahakama Kuu iliamua kuwa, wafanyakazi waliofungua kesi ya awali ndio walipwe madai yao, na kwamba deed of settlement iliyosajiliwa Mahakamani ilihusisha wafanyakazi hao pekee” alifafanua Dkt. Kijaji.
Alisema
wafanyakazi wengine ambao hawakuwa sehemu ya kesi hiyo hawawezi kulipwa
kwa kutumia hukumu na tuzo ya kesi ambayo hawakuwa sehemu yake na
kusisitiza kuwa, Serikali haiwezi kulipa madai mengine ambayo
hayakuthibitika kisheria.
0 comments:
Post a Comment