Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kongwa, White Zuberi kwenye semina iliyoandaliwa na mradi wa The
Foundation for Civil Society wilayani hapa.
Alisema katika msako huo, wazazi na walezi wenye watoto ambao ni
walemavu watakaobainika kuwaficha watoto wao majumbani katika kipindi
cha uandikishaji wa shule watachukuliwa hatua kali pamoja na kufikishwa
mahakamani.
Akifungua semina ya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya rasilimali
za umma kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum iliyofanyika wilayani
Kongwa, alisema wilaya hiyo imekuwa na changamoto kwa upande wa wazazi
na walezi wenye watoto ambao ni walemavu.
Alisema bado kuna kundi kubwa la watoto wenye ulemavu ambao
wananyimwa fursa ya kupata elimu, hivyo kwa kushirikiana na jamii
watafuatilia majumbani watoto hao ili waweze kupelekwa shule na
kuandikishwa. Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Dodoma (TKB),
Omary Lubuva alisema, ipo haja ya wazazi kuona umuhimu wa kuwapeleka
watoto wenye ulemavu shule ili waweze kuja kuwa msaada mkubwa wa kupiga
vita umaskini katika kaya.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment