Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A.
Mwalimu (Mb), (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (katikati) wakati
alipowasili kufungua Mkutano wa Mwaka wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo
ya Jamii unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A.
Mwalimu(Mb), akisalimiana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw.
Patrick Golwike wakati alipowasili kufungua Mkutano wa Mwaka wa wataalam
wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha
Mipango Mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akitambulisha washiriki wa
Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2017
unaofanyika Chuo cha Mipango mkoani Dodoma na kujumuisha Maafisa
Maendeleo ya Jamii ngazi ya Taifa, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri
za Mitaa na wawakilishi kutoka Sekta na Mashirika mbalimbali nchini.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Elimu Bw. Tikson Nzunda akifafanua
neno wakati wa Mkutano MKuu wa Kitaifa wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii
kwa mwaka 2017 unaofanyika Chuo cha Mipango mkoani Dodoma kuhusu umuhimu
wa kuwatumia wataalamu wa Maendeleo ya Jamii katika utekelezaji wa
miradi ya maendeleo yao.
Katibu
Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga
akitambulisha malengo ya Mkutano Mkuu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii
2017 na kumkaribisha Mgeni rasmi Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu kufungua
Mkutano wa Mwaka wa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A.
Mwalimu(Mb) akisisitiza maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kuamsha ari ya
wananchi kushiriki katika shughuli za kimaendeleo kuelekea uchumi wa
Viwanda wakati akifungua Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Mandeleo ya
Jamii unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma.
Baadhi
ya Maaafisa Maendeleo ya Jamii wakisikiliza maelekezo ya Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A.
Mwalimu(Mb)(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wataalam wa
Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini unaofanyika katika Ukumbi wa Chuo
cha Mipango Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A.
Mwalimu(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya Rais
TAMISEMI mara baada ya kufungua Mkutano wa wataalam wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii Mjini Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A.
Mwalimu(Mb) (katikati) akijadiliana jambo na Naibu katibu Mkuu Ofisi ya
Rais TAMISEMI Elimu Bw. Tikson Nzunda (kulia) mara baada ya kufungua
Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Mjini Dodoma kushoto
ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba
Nkinga. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Serikali
imewataka Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kurejesha ari na hamasa ya
jamii kushiriki katika kazi za maendeleo ili kutoa mchango katika
kufikia Tanzania ya Viwanda na yenye uchumi wa kati.
Kauli
hii imetolewa MJini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu wakati akifungua Mkutano
Mkuu wa 12 wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unafoanyika katika ukumbi wa
Chuo cha Mipango Dodoma.
Mhe.
Ummy Mwalimu amesema kuwa kupitia Mkutano huo Wataalam wa Maendeleo ya
Jamii wanatakiwa kutoa mapendekezo kuhusu mbinu bora zitakazosaidia
kurudisha ari na hamasa ya jamii kushiriki katika maendeleo na hivyo
kusaidia kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.
Mhe.
Ummy Mwalimu amefafanua kuwa wataalam wa maendeleo ya jamii ndiyo wenye
jukumu la kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya kisekta hususan kilimo,
afya, elimu, na miundo mbinu na kadhalika.
“Wataalam
wa Maendeleo ya Jamii watumie fursa hii kujitathmini ili kupata majibu
ya namna bora ya kutekeleza majukumu yao ya kuamsha ari ya wananchi
kushiriki kwenye uzalishaji na kutokomeza ukatili wa jinsia ambao
unapunguza kasi ya kufikia uchumi wa kati na maendeleo jumuishi” alisema
Mhe. Ummy.
Waziri
Ummy ameeleza kuwa Kaulimbiu ya Mkutano wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii
kwa Mwaka 2017 ambayo ni “Amsha Ari ya Ushiriki wa Wananchi Kufikia
Uchumi wa Viwanda” inatafsiri azma ya Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya kuwa na Tanzania ya Viwanda ili kufikia uchumi wa kati.
Naye
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba
Nkinga amesema kuwa katika awamu ya sasa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii
wana wajibu wa kuelimisha na kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi za
uzalishaji kwa bidii kwa kuzalisha mali ghafi zinazohitajika na viwanda
na kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo na vya kati.
Bibi
Sihaba Nkinga amefafanua kuwa malengo ya Mkutano huo umezingatia
tathmini ya mchango wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii katika kuamsha ari
na hamasa ya wananchi kushiriki na kuchangia maendeleo kwa kushirikiana
na viongozi wa Sekta na Idara nyingine katika utekelezaji wa miradi ya
maendeleo.
Naye
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amewaasa Wataalamu
wa Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na wadau kutoa elimu na
kuhamasisha wananchi kujitoa katika kufanya kazi za kujiletea maendeleo
katika maeneo yao.
Lengo
la Mkutano huu wenye kauli mbiu isemayo “Amsha Ari ya Ushiriki wa
Wananchi Kufikia Uchumi wa Viwanda” ni kuhakikisha Wizara na wadau
wanashirikiana katika kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi za maendeleo
na kusimamia Mpango ya kutokomeza ukatili wa jinsia ambao kwa kikasi
kikubwa unapunguza kasi ya Taifa kufikia uchumi wa viwanda.
0 comments:
Post a Comment