Msemaji
wa upinzani wa Wizara ya Katiba na Sheria, Ally Salehe amesusa kusoma
maoni ya upinzani ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali baada
ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kukataa kusomwa kwa baadhi ya
maneno yaliyomo katika maoni hayo.
Salehe
alikuwa akisoma maoni hayo leo Januari 30 mwaka 2018 kwa niaba ya
msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu aliyeko nchini
Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi Novemba 7 mwaka
jana.
Maneno yaliyozuiwa na Chenge kusomwa na upinzani ni kuhusu matukio ya uhalifu nchini, likiwemo la kushambuliwa kwa Lissu.
Salehe
alianza kusoma maneno hayo lakini alipofika aya ya nne alikatizwa na
Chenge akimtaka asubiri, baadaye kumueleza kuwa lugha iliyotumika katika
ukurasa kwa kwanza na pili wa hotuba hiyo si ya kibunge.
Baada
ya kauli hiyo, Salehe amesema upinzani unaiamini na unaisimamia hotuba
hiyo kwa kuwa wabunge wote wanayo nakala yake, akaomba kuiwasilisha na
kurejea kuketi.
0 comments:
Post a Comment