Kaimu
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Marcel
Katemba (wa tatu kulia)akifungua kikao baina ya Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali (NGOs ) na Serikali kilicholenga kujadili mpango wa pamoja
katika utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na
Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, kilichofanyika Makao Makuu Dodoma
tarehe 30.1.2018.
Katibu
wa kikao cha ushirikiano baina ya Serikali na wadau wa Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali (NGOs) Bi. Tausi Mwilima (kulia)akisoma Muhtasari wa
kikao kilichopita kwa wajumbe wakati wa kikao cha pamoja moja
kilicholenga kujadili mpango shirikishi wa utekelezaji wa Sera
mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii ili kuharakisha Maendeleo na Ustawi wa Jamii.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike(kulia)
akiwasilisha taarifa fupi juu ya Mpango wa Kuamsha Ari ya wananchi
kujitolea katika kufanya shughuli za maendeleo wakati wa kikao kati ya
wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali(NGOs )na Serikali kilicholenga
kujadili mpango shiriki na endelevu wa utekelezaji wa Sera mbalimbali
zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Slyvia Siriwa(kulia)
akiwasilisha mada kuhusu uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi na utekelezaji
wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto
wakati wa kikao kati Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) na Serikali
kilicholenga kujadili mpango ushiriki wa utekelezaji wa Sera mbalimbali
zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai(kushoto)
akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa kutokomeza
Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa kikao kati ya wadau wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs )na Serikali kilicholenga kujadili
utekelezaji shirikishi wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa
na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Afisa
Ustawi wa Jamii Bw. Twaha Kibalula akiwasilisha mada kuhusu
uimarishwaji wa mifumo ya Ustawi na utolewaji wa Huduma za Ustawi wa
Jamii wakati wa kikao kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs )na
Serikali kilicholenga kujadili ushirikiano na utekelezaji wa Sera
mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii.
Mwakilishi
wa Shirika la World Vision Bi. Janeth Edison akitoa mrejesho kutoka
katika Taasisi yao kuhusu utekelezaji wa Makubaliano (MoU) baina ya
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wadau wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) wakati wa kikao kati ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali (NGOs )na Serikali kilichofanyika makao Makuu
Dodoma kujadili ushirikiano na utekelezaji wa Sera mbalimbali
zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Mwakilishi wa Kigamboni Community Bw. Rashid Kombo(katikati) akitoa
mrejesho kutoka katika Taasisi yao kuhusu utekelezaji wa Makubaliano
(MoU) baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na
Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) wakati wa kikao kati ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) na Serikali kilichokutana mjini
Dodoma kujadili ushirikiano na utekelezaji wa Sera mbalimbali
zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Mkurugenzi
wa Shirika la REPSSI Bibi Edwick Mapalala akitoa mrejesho kutoka katika
shirika lake kuhusu utekelezaji wa Makubaliano (MoU) baina ya Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali (NGOs) wakati wa kikao kati ya Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali (NGOs)na Serikali kilicholenga kujadili ushirikiano na
utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu
ya Maendeleo ya Jamii.
Mwakilishi
wa Shirika la JSI Bi Victoria Munisi(katikati) akitoa mrejesho kutoka
katika Taasisi yao kuhusu utekelezaji wa Makubaliano (MoU) baina ya
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wadau wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) wakati wa kikao kati ya pande hizo
mbili kilicholenga kujadili ushirikiano wa pamoja na utekelezaji wa
Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu ya Maendeleo
ya Jamii.
Baadhi
ya wajumbe wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa
kikao kati ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs )na
Serikali kilicholenga kujadili utaratibu bora wa ushirikiano na
utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na kuratibiwa na Idara Kuu
ya Maendeleo ya Jamii.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
0 comments:
Post a Comment