Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma.
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswaada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya Utumishi wa Umma,
Sura ya 298 (The Public Service Act) itakayowezesha muda wa kustaafu
kwa Wahadhiri waandamizi, Maprofesa na Madaktari Bingwa kuwa miaka 60
kwa hiari na lazima miaka 65.
Akizungumza
wakati akiwasilisha muswaada huo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.
George Masaju amesema kuwa marekebisho katika jedwali yanapendekeza
kuongezwa kwa kifungu kipya cha 25A ambacho kinaainisha kuhusu umri wa
kustaafu ambapo kwa sasa sheria ilivyo haina masharti hayo isipokuwa
umri wa kustaafu umetajwa katika sheria zinazoanzisha mifuko ya hifadhi
za jamii.
Aliongeza
kuwa, uzoefu umeonyesha kuwamba Maprofesa na Wahadhiri waandamizi wa
vyuo Vikuu vya Umma pamoja na madaktari Bingwa wa Binadamu wa
Hospitali za Umma wamekuwa wakihitajika kuendelea kutoa huduma, utaalamu
na uzoefu wao licha yakufikisha umri wa miaka 60 kwa sasa ya kustaafu
na hivyo kulazimika kuajiriwa na Serikali kwa mikataba.
Hatua
yakuwaajiri wataalamu hao kwa mikataba baada ya kustaafu imetajwa
kuongeza gharama kubwa kwa Serikali ambapo muswaada ulipitishwa
unawezesha Serikali kuokoa Kiwango kikubwa cha fedha zilizokuwa
zikitumika katika kuwalipa wataalamu wao mara baada ya kustaafu ili
waweze kufanya kazi kwa mikataba.
Kwa
upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknplojia mhe. Profesa Joyce
Ndalichako alisema kuwa anaunga mkono hoja yakuongeza umri wa kustaafu
kutoka miaka 60 kwa lazima hadi 65 na kutoka miaka 55 kwa hiari hadi
miaka 60.
Aliongeza
kuwa Serikali inayo mikakati ya makusudi yakuwaendeleza wataalamu wa
kada zenye uhaba wataalamu wabobezi ili kuziba pengo lililopo.
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wake wa 10 kikao cha 1
limepitisha muswaada wa marekebisho ya sheria mbalimbali nne ambazo ni
Sheria ya Ufilisi, sura ya 25, Sheria ya Bajeti, sura ya 439, Sheria ya
Ardhi, sura ya 113 na Sheria ya Utumishi wa Umma, sura ya 238.
0 comments:
Post a Comment